Masaa 24 tu baada ya  Yanga kupigwa mabao 3-1 dhidi ya wapinzani wao Simba, uongozi wa klabu hiyo umemfungashia virago kocha wake Ernie Brandts, kufuatia uamuzi wa kikao cha kamati ya utendaji ya Yanga iliyoketi muda mchache baada ya mchezo wao na Simba. 

Mwenyekiti wa kamati ya usajili Abdallah Binklebu amesema leo jijini Dar es salaam kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya kupokea maoni ya wachezaji mbali mbali wa zamani kuhusu kiwango cha timu. 

 "Tumempa notisi ya siku 30 ili tuendelee kutafuta kocha mwingine, na tupo kwenye mchakato wa kumlipa stahiki zake, tuachane kwa amani. 
 “Mwanzoni alipandisha kiwango cha timu, kilipanda sana, lakini baadaye kiwango kikaanza kushuka, tukasema tumpe muda kidogo, lakini tunaona mambo yanazidi kuharibika, hivyo tumeamua kuachana naye kwa sababu hana jipya, sisi tunalenga michuano ya kimataifa zaidi sasa kwa kiwango hichi hatutafika mbali ni lazima tuchukue hatua za haraka zaidi,”alisema. 

 Kuhusu Wajumbe wengine wa benchi la Ufundi, Bin Kleb alisema kwamba taratibu nyingine zinafuata na ndani ya wiki hii kuna maamuzi mengi makubwa ambayo klabu yake itayafanya. 
 Hata hivyo tayari Brandts alikabidhiwa barua yake ya kusitishiwa mkataba rasmi juzi na jana baada ya mazoezi Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga alikutana na wachezaji na kuzungumza nao kwa zaidi ya nusu saa. 
Kocha Brandts amesema  kwa kifupi "Nasubiri notisi ya siku 30 imalizike. Kuna kitu nitaongea lakini sio sasa. Sasa hivi msikilizeni Abdallah (Binkleb) anachosema ukifika muda na mimi nitazungumza."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. hivi tatizo ni kocha au wachezaji wa kitanzania??hivi si ndio hawa hawa wachezaji wakiwa timu ya taifa na kocha mwingine wanafungwa na kutolewa kila mashindano wanayoshiriki??

    ni hivi hao wachezaji watu wazima wa tz hawafundishiki..Yanga na timu nyingine kama mnataka kuona matunda wekezeni kwenye timu za vijana msubiri angalau miaka mitano bila kufukuzafukza makocha then mtaona matunda yake!

    Nimeamini taifa la tz siku hizi watu wake ni wagumu sana kufikiri..yaani hao viongozi badala ya kufikiri in detail wao wanawaza sababu ya kufungwa mechi moja ndio wanamfukuza kocha...aibu sana hii..akili matope kweli kweli

    yanga damu - USA

    ReplyDelete
  2. Tatizo ni Kocha na usajili mmbovu. Kwani hawaoni wachezaji kutoka timu nyingine mpaka wawe wanasajili wachezaji wa Simba tu? AAAGHR!

    ReplyDelete
  3. Mhh ! Jamani kama kwa mechi ya Bonanza au sijui fete tunafukuza kocha,je kwenye ligi si tutafukuza hadi wanachama? Mimi kama Yanga, naona hapa munawapa nafasi watani wazidi kutamba.

    Kila mwaka kocha, hutufiki popote. Kumbukeni tunaongoza ligi, na ni sisi mabingwa waetetzi amabo usajili wetu ni mkubwa. Ni mambo madogo tu tungesubiri.

    ReplyDelete
  4. Mimi ni Yanga damu lakini sijafurahishwa na kitendo cha kumfukuza kocha. Kosa si la kocha bali ni Kaseja na wacheaji wengine walionunuliwa. Mlimisajili Kaseja wa kazi gani?

    ReplyDelete
  5. Imetosha bwana kocha mzito kufanya maamuzi hasa timu inapofanya vibaya na kwa hakika mimi ananiboa kwa hilo!

    sesophy

    ReplyDelete
  6. Vipi kama Yanga ingeshinda?bado kocha angeondoka?kwanini hakufukuzwa kabla ya mechi?kufungwa au kufunga kupo na lazima tuelewe hivyo..

    ReplyDelete
  7. Kweli baadhi ya watz tuna uwezo mdogo sana wa kufikiri. Ni viongozi hao hao waliomtafuta huyo kocha na kumwandikia mkataba mzuri. Leo mkataba unavunjwa kwahiyo lazima alipwe. Kocha mwingine anayeytafutwa naye atapewa mkataba na malipo. Haya yote yanatokea baada ya kupoteza mchezo mmoja tu. Kama timu ingeshinda mchezo huo, yote haya yasingetokea. Wachezaji wanapochuliwa wakubwa, ni vigumu sana kuwafundisha (hawafundishiki) na mtu wanayemuelewa. Sasa ukiwaletea mtu wasiyemuelewa inakuwa ni addition of fuel to the existing fire. Inakuwa ni mchanganyiko wa bangi, gongo na mihadarati. Viongozi wenye uwezo mdogo wa kufikiri wanachukuwa wachezaji (watu wazima) ambao hawawezi kuzungumza lugha ya kocha, na kocha mabye hawezi kuzungumza lugha ya wachezaji unakuwa unatengeneza mlipuko. Mpira unaanza na wachezaji wadogo guys, don't you get it?

    ReplyDelete
  8. Huwezi kucheza mpira kwa kunywa chai na mandazi, ugali na dagaa, wali na maarage, ndizi na utumbo wa taulo, biliani na kachumbali, cocacola na pepsi. Vyakula tunavyokula havitujengi kuwa wachezaji, hata kama tungefundishwa tukiwa bado wadogo. Hii siyo tu kwa mpira wa miguu, ni michezo yote. Mwangalieni Hasheem Thabit navyotia huruma. Ndhani si vibaya tukiwa washangiliaji. Tuwachie mataifa mengine wacheze.

    ReplyDelete
  9. Ukweli ni kwamba timu zetu za hapa nyumbani hazina mipango/mikakati endelevu strategic & progressive plans ambayo itazifanya kuimarika as they go along.kutokuwa na mipango km hiyo kumefanya timu hizi kucheza mipira ya kubahatisha, kwa kuendelea na utaratibu wa kurecycle wachezaji nasio kuwajenga kuanzia chini.Vilex2 timu zinaendeshwa kisiasa zaidi kuliko kisayansi...

    ReplyDelete
  10. Martin ChachaDecember 24, 2013

    Jamani lawama zenu ni too much na wengi mnafikiri amefukuzwa kwa mechi ya juzi tu, si kweli mchakato wa kumsoma na kuangalia anakitu gani kipya ulishaanza toka muda mrefu na timu pamoja na kuongoza ligi imekosa ubora kulingana na wachezaji ilionao kwa muda mrefu saaana, kama mnakwenda mpirani mtakuwa mashahidi, pia hata timu ikitokea imezidiwa kubadilisha/kufanya sub ambazo zitainusuru timu ameshindwa kwa muda mrefu, hongera uongozi kwa uamuzi mzuri na wakati sahihi atafutwe mwalimu mwenye uwezo mkubwa zaidi yake tunaenda kwenye mashindano makubwa sana ya ligi ya mabingwa wa Afrika kwa Brandts tusingefanya cha maana tena, kama mnakwenda mpirani niwakumbushe tu mechi ya Azam, ya Simba mwaka jana ya 3-3, na Hata ya Ruvu shooting tuliyoshinda moja kwa juhudi binafsi za ngasa na Kiiza, timu imechemsha muda mrefu na hana mbinu tena
    Mdau wa Yanga-Martin Chacha Iringa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...