Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeonyesha tena njia kwa wadau wa sekta mbali mbali kwa kuvuka tena mipaka na kueneza elimu kwa wajasiriamali wa Tanzania washiriki wa maonesho maarufu yajulikanayo kama Jua Kali Exhibition ambayo hufanywa mara moja kwa mwaka katika nchi za umoja wa Afrika ya Mashariki.
NSSF imeshiriki kwa mara ya nne katika maonesho haya kwa nia ya kuongeza wigo wa wanachama katika mfuko huo. Shirika hilo linatoa mafao saba kwa mujibu wa tamko la Kimataifa la Shirikisho la Kazi Duniani (ILO).
Mafao haya yakiwemo ya matibabu bure kwa Mwanachama na wategemezi wake, mafao ya Kuumia kazini, mafao ya uzazi, na Mikopo kwa wanachama hutolewa wakati wakiwa kazini na mafao ya muda mrefu kwa mtindo wa pensheni hutolewa pindi vigezo vikikamilika. Pensheni husika ni ya Uzeeni, ya Ulemavu na ya Urithi.
Mafao haya ya Muda mfupi hayapunguzi kiwango cha Pensheni itakayotolewa itakapojiri. Meneja Kiongozi wa Uhusiano wa Mfuko huo, Bi Eunice Chiume alinukuliwa akieleza haya katika maonesho haya muhimu ya wajasiriamali.
NSSF inawatangazia FURSA mbalimbali wadau wote wa sekta binafsi wakiwemo wajasiriamali zinazopatikana kwa kujiunga na uanachama wa Shirika hili.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Batilda Burian akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la NSSF huko jijini Nairobi katika maonesho ya kikanda ya wajasiriamali yanayojulikana kama Jua Kali/ Nguvu Kazi exhibition.NSSF Tanzania imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na wajasiriamali ili kuongeza zaidi elimu kwa wajasiriamali kuhusu Mfuko huo wa Hifadhi ya Jamii pamoja na mafao yake yakiwemo ya matibabu, uzazi, kuumia kazini na Mikopo ya SACCOS. Balozi alitoa pongezi kwa Shirika hili pamoja na Taasisi za MKURABITA, TFDA, TanTRADE zinazoshiriki kutoka Tanzania chini ya Wizara ya Afrika Mashariki na Wizara ya Kazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...