Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Engineer Felchesmi Mramba kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Desemba 2, 2013, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Florens Turuka inasema kuwa uteuzi huo umeanza leo hii.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
2 Desemba, 2013
Hongera sana Engineer Mramba kwa kuteuliwa kwako na imani ambayo Hon. JK amekuwanayo kwako.
ReplyDeleteAidha, tunajua kuwa kuendesha mashirika kama TANESCO katika nchi za uchumi kama wetu hapa Tanzania ziko changamoto za aina nyingi...lakini ukimudu kuzikabili changamoto hizo kwa hekima na uzalendo huku ukimtanguliza Mungu na kuwajali wa - Tanzania ambao kimsingi ndiyo wateja wako, utafanikiwa sana.....
congratulations!
Congratulations Eng Mramba. Panga timu yako iwe kama ile ya NHC ya Nehemia Mchechu.
ReplyDeleteHongera sana Eng.Mramba tunaujua utendaji wako.Rais hajakosea kukuchangua.chagamoto zipo nyingi kwenye shirika lakini tunavyokujua utapambana nazo.mungu akubariki sana
ReplyDeleteCongratulations Eng. Mramba. Hakikisha mgao wa umeme kwisha. Hapo utakuwa umepaweza kabisa. Kisha hakikisha utoaji wa service line hauchakachuliwi na wajanja
ReplyDeletehongera Eng. Mramba tanesco libeneke lile lile, aluta continua ulaji, mdau alex bura dar,
ReplyDeleteEng.Mramba ni wakati sasa wa kulirekebisha Shirika lenye muundo uliopitwa na wakati.
ReplyDeleteNi wazi ya kuwa ukubwa wa Shirika na changamoto za ongezeko la mahitaji vinatoa nafasi kwa WIZI na UFISADI hivyo Shirika ligawanyike kwa Majukumu kama yanavyokuwa Mashirika yenye Ufanisi Duniani kwa mpangilio wa Makundi matatu (3) ya Kiutendaji yanayo jitegemea kama hapa chini:
1.Uzalishaji Umeme (Energy Generating)
2.Usambazaji Umeme (Transmisions)
3.Uuzaji na Ugawaji (Distribuion and Sales)
Pia ziangaliwe njia zingine za kuboresha Huduma kwa UNAFUU WA GHARAMA, UHAKIKA WA UMEME, UBORA WA HUDUMA ZA VINWANGO VYA NISHATI kwa kufanya haya hapa chini:
1.ENERGY DIVERSIFICATION AND ENERGY POOL.
Kuangalia uwezekano wa kuunganisha Umeme na vyanzo mbadala tofauti na utegemezi wa chanzo kimoja cha nishati.
2.ENERGY TRADING.
Kuuingiza Umeme katika Mfumo wa Masoko na kuweza kualika Wawekezaji na Mitaji ya kutosha kwa Fedha za Uendeshaji kama kuliingiza Shirika ktk MASOKO YA Hisa DSE.
We are praying for you and all above you and under you. Be courageous and be blessed and GOD bless Tanzania.
ReplyDeleteHongera! Naungana na wadau wote hapo juu. Ndugu, cheo ni dhamana; na dhamana yako kubwa ni kututumikia sisi wananchi. Kero zetu ziwe ndio changamoto kwako. Kwa kuanzia anza na kitengo cha Emmergency kifanye kazi kama ilivyomaanishwa siyo kulala na kuzunguka hovyo mitaani na magari yakiwa yamebeba mikaa, madumu ya maji wakati wananchi hawana umeme taarifa ziko ofisini kwao toka jana yake, mpaka tunakabana nao mguu kwa mguu ili waende kutatua matatizo. Pili, suala ya kuWEKEWA LUKU mpya badala ya zile za zamani kwa mimi yapata mwaka wa tatu, kila nikitoa taarifa pale Mikocheni na jina unaandikwa ila ukienda kukumbusha cha kushangaza wakiangalia uliandikisha jina halionekani Mkuu chunguza hili huenda kuna Register mbili, na ukiuliza vipi inatakiwa nitoe hela utasikia wanajibu hapana LUKU ni bure na ziko nyingi khaa! mbona hatubadilishiwi? Tatu, hakikisha umeme unasambaa kila sehemu ili gharama iweze kuwa nafuu si kupandisha kwa hao walionao kila kukicha, soko la umeme bado ni kubwa; kwa mfano issue ya nguzo napo ukiuliza utasikia nguzo zipo nyingi zimekuja, sasa kama ndivyo watu wamelipia toka Jan leo tupo Dec na wapo hapa Dar tena Kinyerezi mbona mnawanyia kama sisi wa Mbeya ambao tupo mbali na Dar!!! Viongozi ndio mtakao fanya BIG RESULTS NOW ionekane positive au negative kwa wananchi.
ReplyDelete