Home
Unlabelled
SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WATANZANIA,TAREHE 31 DESEMBA, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Jamani atakapo ondoka Ikulu tutamkumbuka sana Raisi Kikwete!
ReplyDeleteItatugharimu kumpata Raisi atakayeumudu Muungano wa Afrika ya Mashariki EAC yenye Mawimbi na Mashaka mengi, huku ikiwa kama Msafara wa mamba kukiwa na Kenge wengi sana Maraisi waliotokea misituni, vigeugeu na wasio aminika hata kwa chembe na wenye mipango ya chinichini mingi ambao inasemekana watakuwa Maraisi wa maisha nchini mwao kama kule Kigali na Kampala.
Kwa Msimamo alioutoa ktk Hotuba yake ya 7 Novemba , 2013 Bungeni Dodoma mimi nilitegemea Muungano umesha vunjika na yeye atatangaza tumejitoa , lakini haikuwa hivyo!
Kwa hali ya ajabu kabisa Raisi Kikwete alibadili mwelekeo wa mawazo yetu tulio wengi, akisema Tanzania haitajitoa ktk EAC.
Kwa kweli Mhe. Raisi Kikwete amekomaa sana kila idara, ndio maana wahenga walisema Simba huweza kuzaa Simba mkali zaidi!
Mwalimu Nyerere alishachoshwa na hii kitu EAC (Afrika ya Mashariki) na inaonekana hakupenda kusikia kabisa kitu hiyo tena baada ya kukatishwa tamaa tokea ivunjike mwaka 1977, lakini NI WAZI RAISI KIKWETE AMEKUWA MKAKAMAVU NA DUME ZAIDI ZAIDI YA BABA NYERERE KWA KUUBEBA MUUNGANO WA EAC UNAO BOA HAKUNA MFANO!
Ni wazi hata waakina Kagame, Museveni na Kenyatta wanatambua ya kuwa Dakitari wa Muungano wa Afrika ya Mashariki ni Raisi Kikwete!!!
Mimi ni mdau wa afya..
ReplyDeleteHii hotuba imepwaya sana katika sekta hii ya afya.
Imenisikitisha sana rais ametumia muda wake katika mambo ya afya kuelezea upasuaji wa moyo na maradhi ya figo ikiwa ni asilimia chache tu ya watanzania ndiyo watakao nufaika na huduma hiyo.
Nilitegemea rais angejikita zaidi kutuelezea ni jinsi gani serikali inawekeza katika kuzui hayo magonjwa watu wasiyapate.
Nilitegemea kauli ya rais kuhusu kuwekeza katika tafiti ambazo zingetuwezesha kutuonyesha sababu ya watu kuungua magonjwa ya moyo na figo.
Vile vile nilitegemea rais angegusia jinsi ambavyo mtanzania wa kawaida atawezeshwa ili kuweza kupata huduma ya afya pale inapohitajika.
Inawezekana kosa si rais, bali ni la waziri wa afya...hivyo basi kuna umuhimu wa kum-expose waziri wetu wa afya ili aelewa mambo muhimu ya afya katika kizazi hiki.
Magonjwa ya moyo, magonjwa ya figo, hospitali ya chuo kipya cha Muhimbili, na other advanced techs..ndiyo vinahitajika, lakini siyo muhimu kama ambavyo tukihakikisha dispensary zetu zote zinatoa huduma karibu kabisa na wananchi, na wananchi wanaweze kuzi-access.
Dunia sasa inaongelea primary health care re-engineering!
Mdau wa pili, unamaana na kwenye usafiri angeongelea waenda kwa miguu na waendesha baiskeli? Na kwenye kilimo angeongelea ni jinsi gani wakulima wanaweza kupata jembe la mkono?
ReplyDeleteMdau wa wa 3. jaribu kuwa muelewa huo usafiri huwezi kuufaidi km huna afya nzuri, unaweza kupelekwa hospitali nzuri kwa gharama kubwa kwa usafiri wa ikulu lakini kama huduma ya afya ni mbovu huwezi kupata nafuu kwakuwa eti ulisafirishwa VIZURI KWENDA HOSPITALI, Mdau wa 2 ninamuunga mkono kwamba alitegemea kusikia habari ya (primery health care) ambayo ndio inamgusa mtanzania yeyote kuanzia chini hadi ikulu. Kwa ujumla Raisi anapo ongelea maendeleo na mafanikio lazima ajikite saaana kwa wananchi wa chini maana wao ndio wengi na ndio wahitaji kuliko tabaka dogo la walionacho.
ReplyDelete