Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa mji wa Rujewa,Mbarali na Vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Barafu mapema leo,mkoani Mbeya.Kinana amesema kuwa Serikali inapaswa kutengeneza njia nzuri na ya haraka ya kuwajibisha Ofisi za Umma ili kuweza kuwachukulia hatua Wafanyakazi wanaofuja fedha za umma ambao ndio walipa Kodi,Kinana ameyasema hayo katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika Lujewa Wilaya ya Mbarali ambayo imetuhumiwa kufanya ufujaji wa fedha za  maendeleo shilingi bilioni 2.4  na baadhi ya viongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo kati ya 2010 mpaka 2012.
 Sehemu ya eneo la mto Mbarali,kama lionekanavyo pichani ikiwa ni mradi wa ujenzi  wa skimu ya umwagiliaji Mwandamtitu,unaohusisha kata tatu za Rujewa,Ubaruku na Imalilo,Wilayani Mbarali mkoani Mbeya,ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake walitembelea mradi huo unaofaa kwa kilimo cha umwagiliaji mapema leo jioniMradi huo ambao umechangiwa kiasi cha shilingi milioni 50 na Wananchi ikiwa ni sehemu ya asilimia 20 ya mchango wa jamii kwa ajili ya uchimbaji wa mfereji mkuu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbarali,Bwa.Adam Mgoyi alieleza kuwa Ujenzi huo haukukamilika kwa wakati kama ilivyokusudiwa kutokana na kukosekana kwa fedha kutoka serikalini kupitia Wizara ya Kilimo,chakula na Ushirika kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi. Mkurugenzi huyo alieleza pia changamoto za Mradi huo wa Mwendamtitu kuwa unakabiliwa na changamoto ya kutopatikana kwa kibali cha matumizi ya maji kinachotolewa na Mamlaka ya Bonde la Mto Rufiji,kutopatikana kwa kibali hicho kunahatarisha umuhimu mkubwa wa uwepo wa mradi huu.
 Mkuu wa Mkoa,Mh.Abbas Kandoro akifafanua jambo kuhusiana na mradi huo wa umwagiliaji kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokwenda kutembelea eneo hilo mapema leo jioni akiwa sambamba na ujumbe wake,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt Asharose Migiro.
 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt Asharose Migiro akiwahutubia wakazi wa mji Rujewa,Mbarali na Vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Barafu mapema leo,mkoani Mbeya.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo jioni Rujewa,Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.Katika mkutano huo Nape aliwatahadharisha wakazi wa eneo hilo hasa vijana kuwa makini na maneno ya Wanasiasa,ambayo baadhi yao wamekuwa wakiwapotosha na kiasi hata kupelekea vurugu ambazo hazina msingi wowote na zinaweza kuepukika iwapo busara ikitumika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mh Kinana na timu yako mnajitahidi sana sana kukiokoa chama ila pia komalia mabilioni ya uswis ili turudishe imani.hao mchwa inabidi waandamwe bega kwa bega na mabilioni ya uswiss.mkikamilisha hilo basi mtufuate.

    ReplyDelete
  2. Kimsingi umefika wakati wa kuelezana ukweli kama ambavyo timu hii ya kinana inafanya hususan kwa viongozi ambao utendaji wao haukidhi matakwa ya wananchi. PIA uendeshaji wa siasa za kistaraabu ni mzuri sana kuliko ule wa kupanda majukwaani na kutusi wengine. Big up Kinaa, Nape, Migiro @ KNM Crew.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...