Naibu Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkutano wa mabadiliko ya Tabianchi (COP 19) amesema kuna ugumu na umuhimu wa mkutano wa mabadiliko ya Tabianchi, na kuongeza kuwa wamekubaliana wawe na mkataba kwa nchi wanachama jinsi ya kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa kwa kiwango ambacho hakitaongeza Madini Joto duniani.
Muyungi alisisitiza kwamba kuna umuhimu wa wanachama kukubaliana kwa maandishi na kuandika mkataba vile vile amesema walikubaliana kutokufuta mkataba mama wa 1992, na umuhimu wa kupunguza Gesi Joto na kuangalia uchangiaji wa tatizo la Madini Joto katika duniani.

Afisa Habari kutoka Kitengo cha Habari Umoja wa Mataifa(UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari katika hoteli ya Holiday Inn juu ya changamoto na mafanikio ya mkutano wa mwisho wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 19) na msimamo wa Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla juu ya masuala ya Tabianchi na Mazingira duniani.
Kutoka kulia ni Mtaalamu wa mambo ya Nishati na Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Abbas Kitogo, Mwakilishi kutoka Youth of United Nations Association (YUNA) Adam Anthony na mgeni rasmi Naibu Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...