Wasomaji wa utenzi Asha Ali Omar,na Asha Ali Mbarouk,wakitoa burudani yao wakati wa sherehe za ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Utaani A,na Chasasa, Wilaya ya Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba,zilizofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika shamra shamra
za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Risala ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Chasasa Utaani A,Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba ,ikisomwa na Mwalimu Mkuu Msaidizi Zaina Omar Othman,leo baada kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,akiwasalimiana wanafunzi na walimu wa Skuli za Sekondari za Chasasa na Utaani A,baada ya kufunguliwa leo, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake kwa Walimu,Wananchi,na Wanafunzi wa Skuli za Sekondari za Chasasa na Utaani A, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Picha zote na Ramadhan Othman,Ikulu


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...