Familia ya mzee Gaspar Tarimo wa Pugu , Dar Es Salaam tunatoa
shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa, na marafiki walioshiriki katika kutufariji
kwa hali na mali wakati wa kipindi kigumu kufuatia kifo cha ghafla cha mpendwa
wetu Donatha (pichani), mke wa Gasper, mama wa
Martha, Michael,Kuki, Jackline, Charles, na Emmanuel, na bibi wa
Lance-Manase kilichotokea usiku wa 31
Oktoba, 2013 katika hospitali ya Hindu Mandal Dar es Salaam.
Mazishi
yalifanyika nyumbani kwao Mahida Uwa, Rombo tarehe 5 Novemba, 2013. Aidha, familia imefarijika mno na uwepo wa
majirani, ndugu jamaa na marafiki na wote waliotutumia salaam za pole wakati wote
wa kipindi kigumu cha majonzi na maombolezo.
Familia imefarijika na inathamini michango ya wote walioshiriki
nasi. Tunapenda kutoa shukrani za pekee kwa Paroko na Waumini wote wa Parokia
ya Pugu na Kigango cha Buyuni, Jumuiya ndogo ndogo Kanda ya Mikongeni, Paroko
na Waumini wote wa Parokia ya Mahida na Jumuiya ya Mt. Agnes ya Uwa, Mahida;
WAWATA, Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jeshi la
Wananchi wa Tanzania, Mbunge wa Rombo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala,
Diwani wa Pugu, Viongozi mbalimbali wa Serikali na Taasisi zake,Wafanyakazi wa
Ubalozi wa Kanada, na Wanafunzi, Waalimu na Viongozi wa Chuo Kikuu Kishiriki
cha MUCCoBS, Moshi pamoja na Bodi ya shule ya Sekondari, Pugu Station.
Kweli
wote mmetuonyesha upendo wa dhati na usioelezeka; tunasema, ASANTENI SANA,
TUNADHANI MUNGU NDIVYO ANAVYOPENDA..
Shukrani pia ziwaendee madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Jeshi,
Gongo la Mboto na Wa Hospitali ya Hindu Mandal Dar es Salaam.
Kwa kuwa sio
rahisi kumshukuru Kila mmoja
aliyeshiriki nasi kwa namna moja au nyingine,
tunaomba wote mpokee taarifa hii kama
shukrani zetu kutoka moyoni kwa upendo wenu kwa familia hii. Mbarikiwe
sana.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE
'.......Mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda. 2 Timotheo 4:6-8



Poleni sana. Pumzika kwa Amani mama yetu.
ReplyDeleteMisa ya shukrani itafanyika tarehe 8 Disemba, 2013 Parokia ya Mtakatifu Francis, Pugu, Dar es Salaam. Wote mnaalikwa.
ReplyDelete