Familia ya mzee Gaspar Tarimo wa Pugu , Dar Es Salaam tunatoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa, na marafiki walioshiriki katika kutufariji kwa hali na mali wakati wa kipindi kigumu kufuatia kifo cha ghafla cha mpendwa wetu Donatha (pichani),  mke wa Gasper, mama wa Martha, Michael,Kuki, Jackline, Charles, na Emmanuel, na bibi wa Lance-Manase  kilichotokea usiku wa 31 Oktoba, 2013 katika hospitali ya Hindu Mandal Dar es Salaam. 
Mazishi yalifanyika nyumbani kwao Mahida Uwa, Rombo tarehe 5 Novemba, 2013.  Aidha, familia imefarijika mno na uwepo wa majirani, ndugu jamaa na marafiki na wote waliotutumia salaam za pole  wakati wote  wa kipindi kigumu cha majonzi na maombolezo.
Familia imefarijika na inathamini michango ya wote walioshiriki nasi. Tunapenda kutoa shukrani za pekee kwa Paroko na Waumini wote wa Parokia ya Pugu na Kigango cha Buyuni, Jumuiya ndogo ndogo Kanda ya Mikongeni, Paroko na Waumini wote wa Parokia ya Mahida na Jumuiya ya Mt. Agnes ya Uwa, Mahida; WAWATA, Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Mbunge wa Rombo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Diwani wa Pugu, Viongozi mbalimbali wa Serikali na Taasisi zake,Wafanyakazi wa Ubalozi wa Kanada, na Wanafunzi, Waalimu na Viongozi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha MUCCoBS, Moshi pamoja na Bodi ya shule ya Sekondari, Pugu Station. 
Kweli wote mmetuonyesha upendo wa dhati na usioelezeka; tunasema, ASANTENI SANA, TUNADHANI MUNGU NDIVYO ANAVYOPENDA..
Shukrani pia ziwaendee madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Jeshi, Gongo la Mboto na Wa Hospitali ya Hindu Mandal Dar es Salaam. 
Kwa kuwa sio rahisi  kumshukuru Kila mmoja aliyeshiriki nasi kwa namna moja au nyingine,  tunaomba wote mpokee taarifa hii kama  shukrani zetu kutoka moyoni kwa upendo wenu kwa familia hii. Mbarikiwe sana.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE

'.......Mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda. 2 Timotheo 4:6-8

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Poleni sana. Pumzika kwa Amani mama yetu.

    ReplyDelete
  2. Misa ya shukrani itafanyika tarehe 8 Disemba, 2013 Parokia ya Mtakatifu Francis, Pugu, Dar es Salaam. Wote mnaalikwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...