![]() |
Marehemu Mama Laurencia Chande |
Familia ya Marehemu Bw & Bibi Boniface
Chande wa Mikocheni, Dar es Salaam wanapenda kutoa shukrani zao za dhati kwa
ndugu, jamaa, marafiki, majirani na wote walioshiriki nasi katika kipindi chote
kigumu cha kumuuguza na hatimae Msiba wa Mama yao mpendwa Laurencia Chande,
aliyetwaliwa Tarehe 5/11/2013 na kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele
tarehe 8/11/2013 katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Shukrani za
pekee ziwaendee wafuatao:-
1. Dr.
Kaduri Mbeni pamoja na wauguzi wote wa TMJ Hospitali
2.
Dr. Robert Moshiro na Dr. Tulizo Shemu wa
Muhimbili Hospital
3.
Dr Henry Mwandolela wa Heamieda Clinic
Upanga
4.
Mama Cecylia Meshack Gawile wa
Mwananyama Hospitali
5.
Chrisant Malege – Muhimbili Hospitali
6.
Fr. Gilbert na Fr. Kasembo wa Parokia ya
Mt. Martha Mikocheni kwa huduma za kiroho walizokuwa wakimpatia Marehemu mpaka
mauti yalipomfika
7.
Wanachama wa Moyo Mtakatifu wa Yesu wa
Parokia ya Mt. Martha Mikocheni kwa sala na maombi.
8.
Wanajumuiya ya Mt. Bernadini Mikocheni
9.
Kikundi cha akina mama wakatoliki
(WAWATA) Mikocheni
10. Jirani
Mr. & Mrs. Moshiro
11. Kikundi
cha Akina Mama wa Mikocheni (Mama’s Group)
12. Kikundi
cha Akina Mama wa Charity Women Group
13. Wafanyakazi
wa Benki ya Dunia, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, AAR, na Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa kwa kutufariji kwa hali na mali katika kipindi chote cha
msiba.
14. Majirani
wote kwa ujumla wa Mikocheni, Drive-Inn na TPDC Flats
Kwa kuwa sio rahisi kumshukuru kila
mmoja wenu,tunawaomba mpokee shukrani zetu za dhati kabisa kutoka moyoni kwani
mmetuonyesha upendo wa hali ya juu na tunawaombea Mungu awabariki sana.
Kutakuwa na Misa ya kumaliza Msiba wa
Mama yetu Laurencia Chande itakayofanyika Tarehe 15/12/2013 Parokia ya Mtakatifu Martha Misa ya Saa 1.00 asubuhi na Saa 3.00
Asubuhi na baada ya hapo chakula cha mchana nyumbani kwa Marehemu kuanzia Saa 7
Mchana.
..Nimevipiga
vita vilivyo vizuri, imani nimeilinda na mwendo nimeumaliza2 Timoteo 4: 6-8
Bwana
alitoa, Bwana ametwaa,
Jina la Bwana Lihimidiwe.
AMINA
Poleni sana Faustina, Prisca na familia yote. Mungu awafariji ktk kipindi hiki kigumu.
ReplyDeleteRest in Peace Mama Chande.
Marina.