Rais wa kwanza Mzalendo na Mpigania Uhuru wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela ‘Madiba’ akiwa ameshikilia viatu vyake ambavyo aliviacha nyumbani kwa Mzee Nsilo Swai alipoingia Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka 1962 akitokea Afrika Kusini ili kuanza harakati za ukombozi.

Mzee Mandela aliahidi kuvichukua viatu hivyo pindi atakaporejea Tanzania lakini katika safari hiyo ndipo alipoishia mikoni mwa makaburu wa Afrika Kusini na kumfunga kwa miaka 27. Viatu hivyo vilihifadhiwa hadi alipotoka na kukabidhiwa kwa Mandela na mjane wa Mzee Nsilo Swai, Bi Vicky Nsilo Swai (pichani kulia)   Desemba 12,1995 Mandela alipotoka gerzani na hatimaye kuwa Rais wa kwanza Mweusi wa Afrika Kusini.

 Rais Kikwete akimtambulisha Mama Vicky Nsilo Swai na Mama Maria Nyerere kwa waombolezaji wakati wa shughuli ya mazishi ya Mzee Mandela kijijini Qunu Afrika kusini Desemba 15, 2015

 Mama Vicky Nsilo Swai na Mama Maria Nyerere wakiwa katika shughuli ya Mazishi ya Mzee Mandela kijijini Qunu
Mama Vicky Nsilo Swai akishangiliwa na waombolezaji kwenye mazishi ya Mzee Mandela wakati Rais Kikwete alipomtambulisha na kueleza historia ya jinsi alivyomkaribisha Madiba nyumbani kwake na kumtunzia viatu vyake, simulizi ambayo ilimsisimua kila mtu aliyekuwepo ukumbini hapo na mamilioni waliokuwa wanaangalia tukio hilo live dunia nzima.

Maandishi ya Mzee Mandela kwa Mama Vicky Nsilo Swai aliyoyaandika kwenye kitabu alichompa kama zawadi baada ya kurudishiwa viatu vyake mwaka 1995

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Wabongo bwana! Hamjui fursa za kibiashara. Hivyo viatu vingebaki Tanzania kama ukumbusho na vingetumika sana kwenye utalii.Cha msingi ilikuwa kuomba ridhaa yake tu. Watu wangetoka huku na kule kuja kuviangalia.

    ReplyDelete
  2. Mdau wa kwanza...You must be very bright.

    Huku Tanzania tupo tunashangilia hotuba ya mweshimiwa kuwa ilifunika siku ya mazishi, na sisi ndiyo tuliompa late Mandela umaarufu.

    Uwa natamani nisingezaliwa Tanzania...

    ReplyDelete
  3. kwani wewe hujafuatilia na kujua kwamba Madiba mwenyewe alivitaka viatu vyake?

    ReplyDelete
  4. Mdau hapo juu umechemsha hiyo inatakiwa ifanyike nchini kwake Africa kusini na sio Tanzania! Usichanganye mambo. Kwenye museum zao SA wavikweke watalii watavikuta hukohuko. Tanzania tuna vitu vingi mno vya kitalii, iweje leo tuweke viatu vya Mzee Mandela? TunaMlima Kilimanjaro ambao wazungu wengi wanadhani upo Kenya tumeshindwa kuutangaza ipasavyo leo utamwambia nani kuna viatu vya Mzee Mandela akuelewe? watasema huo ni utapeli! Mie nadhani tuna vivutio viiiingi mno vya kutangaza. Kiatu mtu kakuachia atakichukua iweje tena ufanye vyako na kwa ajili ya utalii? mie sioni mantiki hata kidogo. Watanzania Mungu atusaidie hata kwenye uelewa wa mambo madogo madogo. Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa nne, naona wewe ndiye unayechanganya mambo. Mdau wa kwanza alichoonyesha ni uwezo mpana wa kufikiria. Aimaanishi kuwa ndiyo basi viatu viwe sehemu ya utalii.

    Ebu tujiulize, zile kambi walizozitumia wa South Afrika, leo hii tumeziweka katika mazingira yapi kutunza kumbukumbu?

    Yaana wewe mdau wa nne naamini kabisa ni kati ya wale ambao wanashangilia hotuba ya JK wakati wa mazishi.

    Tutasema sana mungu ibariki Tanzania na watu wake, lakini kama mawazo yetu ndiyo hayo, hakuna muujiza, watu watakuja, tutawasaidia, then wataondoka na kwenda kuleta maendeleo kwenye nchi zao, then sisi tutabaki kujifisia kuwa tulisaidia.

    Hakuna muujiza ndugu yangu, nikubadilisha mitazamo tu!

    ReplyDelete
  6. Kisicho chako si mali kitu.Wazo la kutaifisha viatu vya Madiba ingetufedhehesha waTz .Huo ungekuwa wizi namba wahed.

    ReplyDelete
  7. Du! Umaskini Wa roho mmbaya? Utu unakwisha kabisa!

    ReplyDelete
  8. Mdau unayesema nimechemsha nafikri wewe ndio umechemsha. Kwa hiyo unataka kutuambia kwa vile tuna vivutio kama mlima Kili na wanyama basi tusiongeze vivutio vingine? Kumbuka watalii wana interests za aina nyingi. Si wote wanavutiwa na Mlima au wanyama. Kuna watalii wanaovutiwa na mambo ya kihistoria au vitu funny. Unapokuwa na vivutio vinavyokidhi matarajio ya watalii wengi una nafasi kubwa ya kujiongezea kipato kwani watakuja wengi.

    Sasa turudi kwenye hoja ya kwa nini viatu vibaki Tz. Viatu hivyo kubaki Tanzania ni ukumbusho aliwahi kuishi Tanzania huku akiendesha mapambano na wakoloni. Na ni historia kwamba alipoondoka aliacha kitu gani cha ukumbusho. Wapo watu watataka kuhakikisha hilo kwa kuona vitu kama hivyo.

    Viatu kubaki SA ni sawa lakini si hivi alivyoacha Tz. Huko SA anavyo vingi tu. Hahitaji kuchukua alivyoacha Tz. Nadhani hata alipokufa ameacha viatu vingi sana ambavyo kama wasaouth wataihitaji watenda kwenye makumbusho ya kijijini kwake.

    Jambo la msingi ilikuwa kumshawishi aridhie kuviacha na aandike ujumbe wowote kwenye hivyo viatu kasha aweke sahihi yake. Picha kama zilivyooneshwa zingepigwa hapohapo wakati anavikabidhi kwa Watanzania. Vingetengenezewa sehemu nzuri ya kumbukumbu yake.

    Si kosa lako ni upeo mdogo wa kuchanganua mambo ulio nao. Huna tofauti na hao wanaoachia wanyama wetu waende QATAR kinyemela huku wakijua kufanya hivyo ni kuzuia watalii wa QATAR wasije Tz.

    Kaka michuzi usibanie hii comment ili tuweze kuelimishana.

    ReplyDelete
  9. Mdau wa viatu umechemsha kwelikweli, with a touch of written diarrhoea.

    ReplyDelete
  10. lakini nadhani wakuu wangu hapo juu msiende mbali sana, inaonekana wote mna hoja ila mnatofautiana kwenye kile kila mmoja wenu anachojaribu kusisitiza.

    Nadhani hoja ya kuwa na viatu vya Madiba TZ siyo mbaya sana & still hata sasa bado vinaweza kurudishwa kwa heshima hii ya nafasi ya TZ kwa SA - hilo linazungumzika kabisa kidiplomasia; lakini pia ukiondoa viatu hata ile nyumba aliyoishi Mandela wakati huo (1962) alipokuja Tanganyika inaweza kufaa ikifanywa sehemu muhimu ya makumbusho kwaajiri ya hii historia kubwa ambayo imeshafanyiwa "promo' ile siku ya mazishi na dunia nzima sasa inajua hilo....kwahiyo hapo milango yote imeshafunguka.

    Pia hata kule kwenye kambi mbalimbali kama Mazimbu, Kongwa etc kunaweza kukaboreshwa na kufanywa aina fulani ya makumbusho; kwakifupi fursa bado ipo na mimi sioni kuwa kitendo cha kurudisha zile "ndopu" basi ndo kabisaa tumepoteza fursa ya kitalii....hapo nadhani itakuwa siyo sahihi sana.

    Hatahivyo, ukiangalia kwa makini utagundua mtoahoja (Mdau wa kwanza) amelitazama hilo kibiashara zaidi....na hayo ndiyo mawazo ya 21stC; yaani kila opportunity unaitazama kwa lengo la kuzalisha faida....namkubali kwa muono huo.

    Mdau wa pili amechanganya kidogo siasa na diplomasia (aliyoshindwa kuijengea hoja madhubuti) amejitahidi naye kiasi fulani japo alihitaji kutohusisha hoja ya Mt. K'njaro kwa vile kwa kufanya hivyo ametoka nje ya wigo kiasi fulani; na pia amesababisha Mtoahoja aje na ukweli kuwa SA kuna viatu vingi zaidi vya Madiba kwanini na hivi navyo virudishwe huko? -

    ReplyDelete
  11. Hivi nyie hamjui kuwa tulidai na kurudisha fuvu la kichwa cha Mkwawa kutoka kwa Wajerumani?

    ReplyDelete
  12. Ankal, ukiona vema wape fursa wadauz wazidi ku-flow na hii mada ya buti za Mzee Madiba hapo front page, au vipi.....naona kama bado iko "hot" vile.

    ReplyDelete
  13. Bado kuna vitu vingi ambavyo vilichukuliwa na wakoloni kupitia wanaowaita wavumbuzi wa Afrika vinatakiwa kudaiwa ili kuboresha talii. dinosour la kusini nk. Vijana mkienda katika museum za Ulaya vitu vingi wamepora kutoka makoloni na kuvifanya vya kwao hiyo ndio kameni iayotakiwa kufanywa ili virudi. Whats viatu vya Mandela.

    ReplyDelete
  14. jamani nashangaa watz. Mandela alisema akirudi atachukua vuatu vyake, sasa iweje vibakie huku kwetu kwenye museum? haina make any sense! kwa kweli hiyo sio njia ya kujenga utalii bora nchini! yaani nimekuja kwako nikaacha pochi yangu nikasema nikirudi toka sehemu Fulani ntaipitia kuichukua halafu uliyeachiwa unaamua kufanya ni yako ikaweke wkenye museum? Does it make sense? kitu sio chako na hata hajakupa consent uchukue then unajifanya unajua ktangaza utalii unakiweka museum,hapo tu kwangu ni tatizo sikubailiani hata kidogo. Kuhusu mazimbu, kongwa nakubali kwa kuwa ni mali yetu! ila ya viatu ni BIG NOOOOOOOO! WIZI MTUPU NA SIO FURSA ZA BIASHARA WALA NINI! SASA AKIJA AKAVIULIZIA UTASEMA NIMEWEKA KWENYE MUSEUM! INA MAANA KILA KINACHOINGIA NCHINI KWETU KIBAKIE KWA KUWA TUNA MUSEUM ZISIZO NA VIATU? TUNAPENDA KUSHOBOKEA VITU VISIVYO VYETU, NASEMA TUNA VITU VINGI KWA AJILI YA UTALII HPA NCHINI!

    ReplyDelete
  15. Ikiwa Mzee Mandela angekuwa hajaja Tz tangu 1962 tungekuwa na sababu ya msingi kusema kwakuwa Madiba alisema akirudi atavichukua viatu vyake na bado hajarudi.....lakini sasa Mandela alikuja Tz mara kadhaa baada ya kutoka jela.....Je, sababu ya kubakisha Tz hizo "buti" bado zipo?

    Au kama tungesema labda hivi viatu tuviache viwekwe National Museum ya Tz, katika kuvielezea kwa hao watakaofika hapo Museum tutasemasemaje hasa?

    Labda nijarubu kidogo: "ooh unajua hizo hapo ni buti za Mzee Madiba, aliziacha kwa kada mmoja wa TANU (Mzee Nsilo Swai) alipokuja 1962 akiamini atakaporudi Tanganyika angevichukua na alipoondoka wakati huo hakuweza kurudi maana alikamatwa na Makaburu na kutiwa gerezani kwa 27 yrs....."

    Swali: kwahiyo tangu atoke jela hajawahi kuja Tz?
    Jibu: "aah...alikuja, ila alisema (labda) viatu vibaki hapa Tz Makumbusho ya Taifa"

    au jibu liwe vinginevyo ....n.k; utaona kama inaleta ukakasi fulani hivi...ni kama tumezing'ang'ania hizo buti ili kutafuta "mtoko" au umaarufu aina fulani kupitia historia ya Madiba.

    Hatahivyo, viatu hivyo vikiwa museum ya SA bado jina la Tz litatajwa huko kwa umuhimu wake katika historia hiyo ya Madiba na kwamba kwa kufanyahivyo bado itatupa fursa ya kutambuliwa na dunia na pengine kuwa kivutio cha aina yake kwa namna nyingine.

    Nadhani tuimarishe tu vivutio vingine vya kwetu vya kitalii....achana na buti za Madiba, viatu! viatu!....mbona hatuzungumzii kiati alichovaa JK Nyerere alipoenda UN kudai uhuru???

    ReplyDelete
  16. kumbukumbu zangu ,hivyo viatu viliuzwa kwenye mnada huko marekani ,na pesa alipeleka kwenye foundation yake ya ukimwi.swala si hotuba tu ukia chini na kujiuliza vema utaona hiyo hotuba imezaa mambo mengi tu.

    ReplyDelete
  17. Hii hoja ya viatu vya bado mwanzo niliona kama mdau hana "Hoja" ila kuna mantiki, kama vingebaki ingekuwa ni sehemu ya kielelezo cha uwepo wake hapa Bongo miaka hiyo.

    Hata hivyo sishangai maana Tz sisi ni hodari wa kuona fursa na kuzi ache zipeperuke.

    Mfano kuna hoja kuwa Nigeria walikuja Bongo kujifunza wazo la kufanya Dodoma Makao makuu ya serikali na waliporejea kwao hilo wazo chap chap wakalifanyia kazi Nadhani waliofika ABUJA wana la kusema,Dodoma yetu bado ni" Mji wa kusadikika"

    NI KWELI HICHO KIATU ILIKUWA NI FURSA YA KIUCHUMI KIAINA!!!

    Wabongo tufunguke jamani, ndio kuna kucha hivyo!

    ReplyDelete
  18. The mdudu,jamani mtu kwao huko Mazimbu ya moro ndiko ntokako naomba serikali ya mkoa ipaboleshe hapo mazimbu ikiwezekana lijengwe gorofa lefu sn zaidi ya 70 ili iwe kichocheo cha uchumi wa mkoa,na mkishindwa nyie wa sasa basi nasubiri 2015 AFANDE SELE atakaposhinda ubunge ntamwandikia barua ili asimamie huo ujenzi wa hilo jengo mpaka likamilike coz tunamwamini mwana moro mwenzetu na mkombozi wa mkoa wetu ni yeye

    ReplyDelete
  19. Mdau tufungue macho zaidi, hii speech ya JK imezaa mambo mengi yapi tena Muheshimiwa? Maana hapo si ndo utatupeleka shule zaidi....funguka basi ili utupe hizo "tips" tafadhali.

    ReplyDelete
  20. viatu vya mandela ni suala dogo sana kubishana nalo ukilinganisha na vivutio lukuki tulivyonavyo, pia mfahamu kwamba masuala haya yanaenda sana na mahusiano ya kimataifa kwa hiyo sio suala la kuchangamkia fursa ya viatu tu wandugu. kuhusu hotuba ya muheshimiwa mimi nimeipenda sana kwa sababu imeamsha hisia za watu kuhusu mchango wa Tanzania katika ukombozi wa nchi za Afrika. kwa vijana waliozaliwa juzi walikuwa hawafahamu nchi yetu ilivyojitoa mhanga katika kulikomboa bara la Afrika. kwa hiyo kusema ukweli hotuba ile nimeifagilia sana.

    ReplyDelete
  21. Nafurahi sana kuona Watz wanagongana kimawazo kwa kupigania ukuwaji wa sector ya utalii na uchumi kwa ujumla. Hii mada nadhani iwekichocheo na changamoto kwa serikali za mikoa na serikali kuu pamoja na taasisi husika ili tuone ni jinsi gani tutaifanyia kazi.

    Hongera mdau ulie zaa hoja hii kwani imeleta changamoto zenginezo katika kukuza utalii wa nchi.Sasa kazi kwenu serikali chukueni hii hoja, kuipuuza ni kudharau maoni ya wananchi wenu.

    TAFAKARI HAKI MAONI

    ReplyDelete
  22. Huyu mama naye nampongeza. Hivi mbona akina vicky wengi wanakuwaga na busara nyingi?

    Viongozi hebu watfuteni hao akina vicky wapewe kazi za mawazilri mizigo muone mambo.
    Hawa akina vicky nafanamu kama 3 vile na wote ni wachapa kazi.

    ReplyDelete
  23. Kina vicky si wachapa kazi tu vile vile ni waaminifu kupindukia

    ReplyDelete
  24. Tanzania nchi yangu.....kazi ipo. Kwa ni huyu mama naye amefanya lipi? Ningemsifu kama angekuwa ameandika kitabu chake kuhusu jinsi alivyokutana na Mandela na sasa hicho kitabu kakiweka sokoni nchi mbalimbali duniani, huku aki-reserve all rights to Swai family.

    Historia ya nchi haiwezi andikwa kwa kutoa hotuba kwenye mazishi!!!! Kwa nini tusiandike vitabu tukauza kote duniani, watu wakavisoma miaka zaidi ya mia.

    Mtu yeyote hasitudanganye, ile hotuba haijazaa kitu chochote, zaidi ya dunia kuelewa kwa nini sisi bado ni maskini.

    Haileti maana kama, tutajivunia tumesaidia ukombozi wa Africa wakati, tumeshindwa kujisaidia wenyewe. Inawezekana watu uja kuomba msaada kwetu kwa sababu ya uwezo wetu mdogo wakufikiria.

    TUAMKE NDUGU ZANGU....



    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...