Wachezaji wa Timu ya Simba na baadhi ya viongozi wao wakipozi na kombe lao baada ya kukabidhiwa kwa kuifunga Timu ya Yanga Mabao 3-1 katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jioni ya leo.Mabao ya Simba yalifungwa na Hamis Tambwe mawili na Ramadhan Singano huku la kufutia machozi la Yanga likifungwa na Emmanuel Okwi.Picha zote na Othman Michuzi.
Meneja wa Yanga, Afidh Ally akipokea mfano wa hundi ya zaidi sh. 98 milioni Kwa kuibuka washindi katika shindano la Nani Mtani Jembe kwa kupata kura nyingi katika unywaji wa bia ya Kilimanjaro.
Hundi ya Simba ilisomeka hivi pamoja na Ushindi Mkubwa walioupata dhidi ya wapinzani wao.
Mgeni Rasmi katika Mchezo huo,Waziri wa Sheria na Katiba,Mh. Mathias Chikawe akikabidhi Kombe la Ushindi wa Nani Mtani Jembe kwa Nahodha wa Timu ya Simba mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa,Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Milioni moja na ushee, dhidi ya milioni tisini na ushee! Tafsiri yake nini?

    ReplyDelete
  2. Ankal wewe uso wako haukukaa kiyanga yanga lakini kumbe wewe ni Yanga mkubwa.
    Badala ya kuzungumzia jambo la maana unazungumzia eti milioni 98. Ndio nini?
    Simba tumeonesha udume wetu mbele ya hao kandambili wako, wewe badala ya kutupamba eti unaonesha hundi.
    Lakini mimi sishangai Ankal. sababu hata hata UK timu tako ni bwawa.
    Sisi wana Arsenal daima tutakuwa wana Simba Sports Club.
    Kajiulizeni leo mmechukua Okwi, sijui Kaseja sijui Ngassa lakini mnyama kasambaratisha kama hana akili uzuri vile.
    Siiiiimbaaaa Oyeeeeeeee!
    Mndengereko Ukerewe

    ReplyDelete
  3. Sisi kama mashabiki na wapenzi wa timu hatuhitaji hela ambazo zinaishia mikononi mwa viongozi. Sisi tunahitaji magoli (ushindi) ambayo ndio raha yetu. Pole mzee wa Yebo yebo.

    ReplyDelete
  4. Tafsiri yake ni kwamba Yanga ni wazuri wa kuokota vizibo vya chupa za Bia kwenye mitaro ya bar mbalimbali.

    ReplyDelete
  5. Loga ameanza vizuri ila nashangaa kuona wachezaji wa Simba wanavaa jezi za kijani na njano kirahisirahisi namna hiyo.
    Naomba mnielimishe, ukubwa wa hundi unategemeana na unywaji wa Kili Lager wa mashabiki husika au inakuwa vipi? Tofauti ya milioni 98 na milioni moja ni kubwa sana.

    ReplyDelete
  6. Tafsiri ya hundi hiyo ni kwanza washabiki wa yanga ni mabingwa wa ulevi au kuokota vizibo vya bia mitaroni. Yanga imekuwa club ya pombe sasa. Endeleeni, sisi tutawaonyesha uwezo uwanjani.

    ReplyDelete
  7. Magoli ya kutosha halafu hayana ubishi, raha tupu!

    ReplyDelete
  8. Ama kweli Simba ni Jembe na Yanga ndio mpini wake!

    ReplyDelete
  9. Jana iljidhihirisha kua mpira na rusha roho ni vitu viwili tofauti. Yanga ikiongozwa na malkia wa rusha roho Bi Hadija Kopa yaani Manji walishia kuziba mdomo baada ya Dakika Tisini. Simba Sports Club ni timu wakati Dar Young African ni taasisi... Simba 3 Yanga 1.. Hahahahaha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...