Inline image 1


TIMU ya Kilimanjaro Stars imefanikiwa kusonga mbele hatua ya Nusu Fainali baada ya kuwatoa Mabingwa watetezi wa Kombe hilo Uganda kwa ushindi wa changamoto ya penalti 3-2 katika michuano ya kombe la Chalenji inayoendelea jijini Nairobi, shujaa akiwa kipa Ivo Mapunda .
Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Manispaa ya mji wa Mombasa,  Uganda ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza likifungwa na Daniel Sserunkuma katika dakika ya 16 akimalizia krosi ya Khamis Kiiza, bao ambalo halikudumu sana kabla ya Mrisho Ngassa kuisawazishia Stars kwa shuti kali  nje ya 18.
Baada ya bao hilo Stars walikuja juu na kufanikiwa kupata bao la pili likifungwa na Ngassa tena kwa mpira wa adhabu uliojaa wavuni katika dakika ya 39, matokeo ambayo yalidumu mpaka mwisho wa kipindi hicho cha kwanza.

Kipindi cha pili Stars inayofundishwa na kocha Kim Poulsen, raia wa Denmark, ilipata pigo katikati ya kipindi hicho baada ya kiungo wake Salum Abubakar 'Sure Boy' kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kucheza rafu, ambapo nafasi hiyo iliwapa nguvu Uganda kupata bao la kusawazisha kupitia Martin Mpuga matokeo ambayo yalibaki hivyo mpaka mwisho wa mchezo na kuzipeleka mpaka kwenye matuta.

Katika mikwaju ya penalti Ivo alikuwa shujaa baada ya kucheza penalti mbili za Waganda ya beki  Khalis Alucho na  ile ya mwisho iliyopigwa na Sserunkuma ambayo ndiyo iliyoivusha stars.
Ifuatayo ni orodha ya waliopiga penalti katika mchezo huo.

Kilimanjaro Stars                                              Uganda
Erasto Nyoni (kakosa)                     Godfrey Walusimbi (kakosa)
Mbwana Samatta (kakosa)                Emanuel Okwi (kapata)
 Amri Kiemba (kapata)                      Khalis Alucho (kakosa)
Athuman Idd (kapata)                        Hamis Kiiza (kapata)
Kelvin Yondani (kapata)                    Sserunkuma (kakosa)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera saana vijana wa Stars haya ndiyo mambo watanzania tunayapenda ushindi..ushindi..ushindi..ushindi
    Matokeo ya mchezo wa mpira wa kisasa kufungwa,droo hazikubaliki.
    Mwalimu Poulsen,benchi zima la wataalamu na wachezaji wote kila la kheri kufika mwisho wa fainal.
    Mikidadi-Denmark

    ReplyDelete
  2. Hongereni Stars mlistahili Ushindi. Nilivyoangalia Uganda walikuwa 12 uwanjani kwa kipindi kirefu sana kiasi kwa kuchangia uchezani wa hasira ulituletea. Mechi ijayo itakuwa ngumu zaidi has kipengele cha mchezaji wa 12.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...