Na Ripota wetu Kanda ya Ziwa
Kikosi kabambe cha Sugar Ray cha Mikocheni, Dar es salaam, kikiwa tayari kupambana na Mwanza ity CVeterans katika uwanja wa CCM Kirumba Jumamosi ambapo Sugar Ray waliibuka washindi kwa bao 3-2. 
 Mabao ya washindi yalifungwa na Abbas Haki "Fumo" dakika ya 10 baada ya kupokea pande safi toka kwa kiungo mchezeshaji anayewaniwa na TP Mazembe, Issa Batenda. 
Mshambuliaji mkongwe Saidi Tully (yuko katika form kama Suarez) aliye-podoksi kea free kick nje ya box baada ya Abbasi kufanyiwa madhambi dakika ya 40. 
 Bao la tatu kafunga Clement Sanga baada ya kupokea pasi murua toka kwa yule yule mgawaji Issa Batenga. Baada ya hapo Mwanza City Veterans wakaja juu, na kufanya mabadiliko ya subs 9, na kufanikiwa kupata magoli mawili, moja likiwa la off side kabisa.
Sugar Rays wakijiandaa na mtanage uwanja wa CCM Kirumba dhidi ya Mwanza City Veterans
 Sugar Rays na Mwanza City Veterans wakisalimiana kabla ya mchezo huo.
 Ni wakati wa mapumziko na wachezaji wa Sugar Rays wakipoza rejeta zao
 Nyota wa Sugar rays Clement Sanga na Saidi Tully wakila pozi huku jamaa akidandia kwa nyuma
 Kiungo mchezeshaji Issa Batenda anayesakwa na TP Mazembe na mwenzie Matare wakitoka uwanjani baada ya gemu. Maajaneti wa timu hiyo ya Congo DRC inasemekana wako Mwanza kujaribu kumchukua Issa, lakini yeye anasita kwa sababu Yanga, Simba na Azam zinamtaka pia.
Hapa wakiwa kambini hoteli ya Isamilo walikofikia kabla ya mchezo. Baadaye meneja wao (huyo dada ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja) akawahamishia hoteli ya Gold Crest kama zawadi ya ushindi.
Sugar Rays wakisherehekea ushindi usiku huu hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza. Safari yao hii imedhaminiwa na Michuzi Blog....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Haya ndiyo mambo yanayotakiwa, sio kila siku vijana wanashobokea masiasa tu. Hongereni Sugar Rays na Mwanza City Veterans kwa kuamua kutembeleana katika sikukuu ya Uhuru. Tunategemea mwakani Mwanza City watatia mguu Dar. Ila wewe Ripota wa Kanda ya Ziwa acha ushabiki. Yaani unasema waziwazi kuwa goli la pili lilikuwa off side kabisa, kwani we refa? Halafu hata majina ya wafungaji wa Mwanza hujaweka. Angalia sana kijana, tutakushtaki kwa mwajiri wako. Tafuta majina ya wafungaji haraka utuwekee hapo...Ohoooo...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...