Wadau wa amani wakiwa jukwaa kuu wakiwa wanafuatilia matukio mbali mbali ya maadhimisho ya kuutakia amani mkoa wa Arusha baada ya kukumbwa na matukio mbali mbali yaliotokea baada ya uchaguzi mkuu na mabomu kwenye kanisa la Joseph mfanyakazi olasit na Soweto mkutano ulioandaliwa na msajili wa vyama vya siasa na vyama vya siasa mkoani hapa na kufanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini hapa.
Mmoja wa washiriki akiwaonyesha viongozi na wananchi wa jiji la Arusha hawapo pichani waliohudhuria hafla hiyo bango lisemalo amani kwanza vyama baadae ujumbe ulioendana na siku hiyo mbele ya msajili wa vyama vya siasa jaji Francis Mutungi na mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo na viongozi wa vyama vya siasa na dini mkoani hapa.
Sehemu ya umati mkubwa wa wananchi na wakazi wa mkoa wa Arusha walioshiriki kuiombea amani mkoa wa Arusha wakifuatilia matukio mbali mbali yaliokuwa yakiendelea uwanjani
Mchungaji Christopher Mwakasege akiombea amani ya mkoa wa Arusha kwenye siku hiyo ya kusahau tofauti na matukio yaliotokea kwenye mkoa huu wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwenye uwanja wa sheikh Amri Kaluta Abeid
Juu na chini wanaonekana viongozi mbali mbali wa serikali, vyama vya siasa na dini mkoani Arusha Pamoja na mgeni Rasmi Jaji Francis Mutungi Msajili wa Vyama vya siasa wakiwa kwenye maombi yaliokuwa yakiombwa na mwalimu na mchungaji Christopher Mwakasege kwenye uwanja wa sheikh Amri Kaluta Abeid.
Picha zote na Mahmoud Ahmad wa Globu ya Jamii, Arusha)


AMANI KWANZA VYAMA BAADAYE!!!
ReplyDeleteUstaadhi hapo ktk Picha ya Pili kutoka juu amebeba Bango lake lipo simple na maneno machache lakini yenye ujumbe mkubwa sana kwa mtu mwenye akili nzuri.
Ni maneno manne (4) tu lakini ni makubwa sana, tuache Ujinga na Upumbavu uliokithiri kwa kushabikia Siasa za machafuko na vurugu zenye kuhatarisha Amani na Ustawi wa jamii yetu!!!
AMANI KWANZA VYAMA BAADAYE!!!
ReplyDeleteUstaadhi hapo ktk Picha ya Pili kutoka juu amebeba Bango lake lipo simple sana na maneno machache lakini yenye ujumbe mkubwa sana kwa mtu mwenye akili nzuri.
Ni maneno manne (4) tu lakini ni makubwa sana, tuache Ujinga na Upumbavu uliokithiri kwa kushabikia Siasa za machafuko na vurugu zenye kuhatarisha Amani na Ustawi wa jamii yetu!!!