Dkt. Reginal Mengi
---
Baada ya Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara ((TNBC) uliofanyika tarehe 16 Desemba 2013, chini ya uenyekiti wa Mhe. Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, sikutegemea kwamba Mhe. Profesa Muhongo angeendeleza mashambulizi dhidi yangu kwa sababu katika mkutano huo ambao ulikuwa na mafanikio makubwa tulifikia maamuzi ya kudumisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta Binafsi, kitu ambacho nimekuwa nikipigania. Hivyo basi, kauli ambazo Mhe. Profesa Muhongo amezitoa Bungeni tarehe 19 Desemba 2013, zimenishtua na kunisikitisha sana.

Ningependa kuwaeleza Watanzania 
wenzangu yafuatayo: BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mmmh,huu sijui niuite ugomvi wa mfanyabiashara/mchumi na mjiolojia au Waziri na Mkurungezi wa IPP?au Dr.Reginald Mengi na Prof.Sospeter Muhongo?!

    Mimi kama mdau wa madini naomba nichangie kidogo kwenye hili Sakata la Wawili hawa.Nimesoma maelezo ya Bwana Mengi na nilibahatakia kuona presentation ya Prof. Muhongo aliyoitoa majuzi kwa mbwembwe nyingi za kijiolojia!Kwa kumsaidia tu Mzee Mengi,Prof.Muhongo kama humfahamu vizuri unaweza kusema ana dharau,kiburi,jeuri n.k lakini ni mtu smart sana(Ni mwalimu wangu UDSM 1994-1997),namfahamu vizuri sana-ingawa anaweza kuwa na madhaifu yake kama binadamu).So Mzee Mengi relax,rest assured vitalu utapata.

    Mengi na Prof Muhongo wote wana hoja.Ninachoomba tu kumwuliza Dr.Mengi atueleze kwanza yeye tangu ameanza utafiti wa madini(Mineral exploration),amegundua kiasi gani cha madini hapa TZ(mineral deposit discoveries)ataje,mfano, hapa niligundua ounces 100 za dhahabu,pale nikagundua tani 2000 za shaba,chuma n.k na hizo gemstones za Mererani ziligunduliwa na kampuni yake?au yeye malengo yake ni yapi?Awe wazi,kama anafanya u-middle man awe wazi kuliko hii style anayotumia ya kutaka kutumia neno "watanzania".Suala la gesi ni gumu kidogo,kwanza hatuna wataalamu wa kutosha wa kutafuta mafuta na gesi hata kama una mifuko imejaa midola bado unahitaji kuwa na "skilled people" kwenye hii Sekta na vifaa vya kisasa vya utafiti wa ama mafuta/gesi kwa ujumla.Suala la wazawa kujiunga(JV) na makampuni ya kigeni nakubaliana na Dr.Mengi lakini je Watanzania wangapi wenye uwezo huo?.Prof Muhongo anaelewa anachokifanya,Watanzania watapewa vitalu watashindwa kuviendeleza.Wawekezaji wa kigeni wana mitaji yenye nguvu(tuwe wawazi),watafanya utafiti kweli kweli tena wa kisasa(wana teknolojia ya kisasa hawa),watalipa kodi watatoa ajira za "kumwaga".Prof.Muhongo,kwa maoni yangu anaweza kutoa asilimia fulani iwe ya wawekezaji wazawa lakini itachukua muda kwa Wazawa kugundua hayo mafuta labda kwa udalali tu hapo sawa.Tunashindwa(WaTZ) kufanya drilling ya utafutaji wa madini ya kawaida mashimo ya mita 200(diamond drilling),itakuwaje hizo deep drilling za mafuta na gesi ambazo zinaenda maelfu ya mita ardhini(zikiambana na modern technology).Sisi bado hatujawa tayari kwa sasa(ni maoni yangu)

    Hii nafasi ni ndogo blog ya jamii nilikuwa na mengi ya kueleza hapa bila kuingiza siasa wala kupendelea upande wowote.Weekend jema wote

    David V

    ReplyDelete
  2. Wajameni, inawezekana kuna chuki kati ya Mengi na Muhongo. Lakini kiukweli, Muhongo amekuwa na kauli tata ambazo haziashirii kuwa ni kiongozi wa umma. Maelezo ya Mengi juu ya uzoefu wa biashara ni kweli tupu. Mtu anayefanya biashara ni mtalaam wa biashara kuliko yule anaisoma biashara na kuiongea tu mdomoni. Kwenye ulimwengu wa leo, unasema Watanzania hawana hela? Kwani hao unaosema wana hela wanazitoa wapi? Hela zipo bank, zipo kwenye hisa, n.k. Ukiwa na viable business idea, unawasilisha business plna yako, ukikidhi vigezo vya kibeni unachukua fedha na kama tatizo ni ujuzi, una-import na kazi zinakwenda. Ni vizuri viongozi wa umma tukatumia busara tunapoongea na Watanzania. Hatujifunzi tu kwa JK? Siku zote JK hata kama mambo ni magumu, hutumia namna ya kuwasilisha ujumbe wake pasipo kumkwaruza mwananchi. Muhongo, tambua wewe ni kiongozi wa umma, rekebisha namna ya kuongea na Watanzania kama unania ya kuitumikia Tanzania

    ReplyDelete
  3. ndugu RM umezungumza mambo mazito sana ambayo kwa sisi walalahoi ikiwa hizi habari ni kweli basi zinauumiza na itakuwa vyema suala hili likazungumzwa bungeni na sio na profesa muhongo kujifanyia maamuzi. Na ni vyema kwa profesa kufikiria maslahi ya raia kwanza , ikiwa wageni watawekeza sio tatizo kama ulivyosema bali ni kwashikisha na wawekezaji wa TZ, Nakupongeza kwa kuzitoa habari hizi, na uwe mkweli daima.

    ReplyDelete
  4. mtoa maoni David naona unaona mbali sana nafikiri tunahitaji mambo kuwekwa wazi kama ulivyosema kuwa masuala hayo ya gesi na mafuta, sisi walalahoi hatujui gharama na ufundi lakini ikiwa hayo uliyosema ni hivyo basi hakuna pingamizi kwa kweli ujuzi hatuna itabidi tuwape wawekezaji wa nje.

    ReplyDelete
  5. Tatizo la Hutu ngugu yetu mengi.kila Ujambo wanaona anaweza au anajua kuna mambo mengine kiukweli awezi kujua.na kitu jingine mazoea hans shida.Hutu dr mengi amezoea comand kwa mawaziri.kitu ambacho anakosea sana.waziri akikataa sera zake.basi ni beef kwelikweli.na kwa kuwa anasehemu ya kuzungumzia.kwenye redio.gazeti.tv basi anasahau Kabisa uungwana ni kujifunza kutoka kwa watu wengine.hivyo vitalu alishawapa kazi hao watanzania anaowafanya silaha?wacha lufulia watanzania kama chambokuwa mkweli ulishasema umepata nini machimbo ya tanzanaite.migodi ya tanga na sehemu zingine.unataka kuwa kama rafiki yako mosha amefungua bank ya akiba bank kwa pesa za Nico huku akisema niko umepata hasara.wacha kuwatumia watanzania kwa lipi huku unawanyonya kwa umasikini WAO.

    ReplyDelete
  6. Kwa mawazo ya watu kama huyo David V. na huyu anonymous wa nne kweli naamini maneno kua ''NCHI HII ILISHAROGWA NA MCHAWI ALIKWISHAFARIKI ZAMANI SANA'' So tutaendelea kuwa ''MISUKULE'' ndani ya nchi yetu mpaka mwisho wa dunia.

    ReplyDelete
  7. naungana na mawazo ya david v hapo juu,mzee mengi anatumia uelewa mdogo wa wananchi ktk mambo hayo kutafuta huruma,kwa kifupi mengi ni mbinafsi na hatetei wananchi kama anavyotaka kutuaminisha....kwanza sio mwadilifu hata ktk makampuni yake tumesikia anawanyanyasa wafanya kazi wake hatoi mshahara mizuri sasa hapa anawatetea akina nani?usitudanganye na vihafla vya kukusanya watoto na kuwapa juice...mengi atueleze ktk hayo maeneo ambayo tayari anamiliki serikali inafaidikaje na kodi kiasi gani? asitumie vyombo vya habari kuchafua wengine...

    ReplyDelete
  8. nafikiri tujaribu kujifunza kwa wenzetu kule mashsriki ya kati , mnafikiri ile petroli inachimbwa na wazawa? ni makampuni ya nje lakini angalia maendeleo walyopata pamoja na hayo petroli katika nchi zao ni rahisi kuliko chips na kuku. La msingi ni usimamizi mzuri wa mapato yatakayopatikana yatumike kwa maendeleo ya raia na sio kumalizikia uswiwi kwenye akaunti binafsi. Kwa kuongezea Nd Mengi umesema umeshafanikiwa kibiashara kwa hio unawasemea wananchi katika hili, ukweli ni kwamba hakuna mfanya biashara au tajiri yoyote yule mwenye kutosheka katika dunia hii kila anachopata hutaka apate zaidi na angelikuwa na njia angemzuilia kila mtu asipate riziki ila kwa kupitia yeye, hii ni asili ya kibinadamu ya uchoyo ambayo humfanya yeye kuendelea na wengine kuangamia , savaival of ze fittest

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...