JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
JESHI LA POLISI TANZANIA

Mnamo tarehe 18/12/2013 majira ya saa tatu asubuhi katika kata ya Malinyi, tarafa ya Malinyi, wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro, kundi la watu kutoka maeneo mbalimbali kijijini hapo walivamia kituo cha Polisi Malinyi kwa lengo la kutaka kuwatoa kwa nguvu watuhumiwa 4 waliokuwa wamekamatwa kwa tuhuma za mauaji.
Katika jitihada za kuhami kituo, askari polisi walitoa tahadhali mbalimbali za kuwataka wananchi hao watawanyike ikiwemo kupiga mabomu ya machozi, lakini wananchi hao waliendelea kukaidi amri hiyo. Katika purukushani hizo za askari kutetea kituo na wavamizi kuendelea kuharibu mali za kituo ikiwemo kukichoma moto, wananchi 3 walipoteza maisha na wengine 3 walijeruhiwa.
Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, ametuma timu maalumu ikiongozwa na Kamishina wa Operesheni na Mafunzo (CP) Paul Chagonja kutoka Makao Makuu ya Polisi kwenda kuongeza nguvu katika Operesheni ya kuwasaka na kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo, ili wafikishwe katika mkondo wa sheria haraka.
Jeshi la Polisi linalaani vikali tukio hilo linaloashiria vitendo vya vurugu na uvunjifu wa amani, tukio ambalo limesababisha vifo na majeruhi pamoja na kujenga hofu miongoni mwa jamii.
Aidha, IGP Mwema ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro hususani wilaya ya Ulanga kata ya Malinyi, kuwa watulivu na kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi wakati uchunguzi ukiendelea, mtu yeyote mwenye taarifa za wahalifu hao anaombwa kutoa taarifa kwenye namba ya simu ifuatayo 0754 78 55 57au katika kituo chochote cha Polisi, ili wahalifu hao waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Mutafungwa!
ReplyDeleteMutafungwa!
Mutafungwa!
Malinyi-Ulanga mnacheza na Polisi?
Fanyeni shughuli zenu kihalali, kama ni mboga 'Kitoweo' ombeni Kibali cha Idara ya Maliasili na Polisi Mkawinde nyama kihalali na kwa Vibali!
Acheni Fujo n Vurugu huku mkiashiria uvunjifu wa Amani na Utulivu.
Nendeni mashambani mweni mkalime na kupakua asali Misituni, Msilete Ubabe na Umwamba ni vile Polisi ina nguvu Mutafungwaaaaa!!!
Polisi ni waonevu sana lakini kwa hili nawalaani wananchi kwa hatua waliyofikia. Chonde chonde wananchi msirudie vitendo hivi. Waacheni polisi wafanye kazi yao. Pale uonevu unapotokea wasilisheni malalamiko yenu kwa wakuu wao wa kazi (RPC, IGP n.k.)mkiwataja moja kwa moja wahusika wa uonevu.
ReplyDeletelakini pia serikali na jeshi ni lazima ijiulize kwanini wananchi wanaanza kuongeza kasi ya kuchukua sheria mikonoin??? kuna sababu sio bure tu. utawala wa mabavu na kutisha huwa hauwi na mafanikio. hiyo ni tahadhari tu natoa
ReplyDeleteNadhani serilkali haiwezi kukiri wazi kuwa kuna tatizo. Lakini mimi nawasaidia kusema kuwa kuna tatizo....tafuteni kiini kungali mapema; tunakoelekea kubaya...ni mbaya sana polisi kutokuheshimiwa na raia (kukosa legitimacy)
ReplyDeleteHiyo ni ishara mbaya sana kwa kuwa polisi inapaswa iwe kimbilio na si adua kwa raia...
Tatizo linaweza lisiwe la polisi ila ni la influence na pressure inazozipata toka kwa elites zinazoifanya polisi isionekane kuwa iko neutral na iko kutenda haki regardless ya power za mtu au watu
Na hii ni sababu ya mfumo wa kijamaa tulokuwa nao muda mrefu ambo uli centralize power