Nahodha wa timu ya taifa ya Wanawake ya Tanzania 'Tanzanite' Fatma Issa akisalimiana na nahodha wa Basetsana, Kaylin Swart kabla ya mchezo wa kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake wenye umri chini ya miaka 20 uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Afrika Kusini ilishinda 4-1.
Vumilia Seleiman akimtoka mchezaji wa Afrika Kusini, Nomonde Nomtsheke.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya wanawake wenye
umri chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’, Shelda Boniface akimtoka beki wa timu ya
Afrika Kusini ‘Besetsana’, Tiisetso Makhubela katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za
Kombe la Dunia la wanawake wa umri huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam jana. Afrika Kusini ilishinda 4-1.
Kumiliki mpira.
Shelda Boniface akimiliki mpira mbele ya beki wa Afrika Kusini, Meagan Newman.
Kikosi cha timu ya Afrika Kusini kiimba wimbo wa taifa.
Kikosi cha Tanzanite kikiimba wimbo wa taifa.
Wachezaji wa timu ya Afrika Kusini walioanza katika kipindi cha kwanza.
Wachezaji wa timu ya Tanzanite walioanza katika kipindi cha kwanza.


Kajipangeni tena dada zetu ndio mchezo
ReplyDeleteKule kwengine koote tulikua tunajidanganya tu.....ivi nikiangalia timu za wanawake huku europe zilivyo kamiligado yaani sipati picha hata hao sijui simba au mtibwa wanaweza wakachezewa nusu uwanja...na ndio wanajiandaa na world cup.....nami naungana na mdau wa kwanza hapo ....wanahitaji maandalizi makubwa mno.....ikiwemo mechi nyingi dhidi ya timu nzuri ili kupima viwango vya wachezaji na si kucheza na watoto wa yule mama mwenye lemba kuubwa kichwani anayelilia maji ya ziwa flani huko kusini.Wale walishakua na frustration zao za kimaisha....
ReplyDeletehawa akina dada au akina kaka? yaani hwafanani kama wadada au mazoezi yamezidi.
ReplyDeleteDuuu Madada wa Afrika ya Kusini nowuuuuma! wanatisha kama njaa!
ReplyDeleteYaani pamoja na Msiba wote mnatugandamiza ndugu zenu sisi Tanzania Mabao 4-1?
Jamani wote sisi ndio tupo kwenye Maombolezo ya Mzee Mandela?
Si mngefanya tu tutoke sare?
Ohhh MNATUFUNGA 4-1 !!!
ReplyDeleteJamani hata katika kipindi hiki cha Msiba wa Mandela tunafungana kama tupo siku za kawaida?