Mtaalamu Mshauri wa Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoendeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchni TASAF Rogelio Gomez Hermosillo akiwa katika kikao cha kujadili zoezi la utambuzi wa kaya masikini katika wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeanza kazi ya kutambua kaya masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi nchini kazi iliyoanza katika mikoa ya Mtwara na Lindi baada ya majaribio kufanyika katika wilaya za Bagamoyo,Kibaha,Chamwino na Bunda kuonyesha mafanikio makubwa, zifuatazo ni baadhi ya shughuli zilizofanywa na Mtaalamu Mshauri wa Mpango huo kutoka Benki ya Dunia ROGELIO GOMEZ HERMOSILLO aliyefanya ziara ya kuona namna kazi hiyo inavyoendelea mkoani Mtwara.
Baadhi ya wawezeshaji katika mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wakiwa katika kikao cha pamoja na Mtaalamu Mwelekezi kutoka Banki ya Dunia Rogelio Gomez Hermosillo ( hayupo pichan)ikatika hafmashauri ya Masasi Mikindani.
Mtaalam wa Mafunzo na Ushiriki wa TASAF Bi.Mercy Mandao Mariki akifafana jambo kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wakishiriki kazi ya utambuzi katika eneo la Chuno Manispaa ya Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara..
Wawezeshaji Ngazi ya halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wakimsikiliza Mtaalamu Mwelekezi wa Mpango wa kunusuru kaya masikini kutoka Benki ya Dunia Rogello Gomez Hermosillo (hayupo pichani) juu ya namna ya kutambua kaya za walengwa wa mpango huo ulioanza kutekelezwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Mtaalam Mshauri wa Mpango wa kunusuu kaya masikini kupitia Mafuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF Rogelio lGomez Hesmosillo aliyeshika tama akisikiliza mchango wa mmoja wa wawezeshaji wa mpango huo(hayupo pichani) wakati wa mjadala wa namna zoezi la utambuzi wa kaya masikini katika halmashauri ya Mtwara Mkindani mkoani Mtwara linavyoendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...