Na Mwandishi wetu, Mbeya

Jumla ya wahitimu 536 wanatarajiwa kuhitimu na kutunukiwa shahada katika mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu Mzumbe, kampasi ya Mbeya leo.

Wahitimu hao ni kati ya wahitimu 3554 katika kampasi zote tatu za chuo hicho kwa mwaka wa masomo wa 2012/2013 ikilinganishwa na wahitimu 3049 mwaka 2011/12.

Kwa mujibu wa Mkuu wa  Chuo, Prof. Ernest Kihanga hicho sherehe hizo zitashuhudia wahitimu katika programu mbalimbali wakifuzu rasmi katika sherehe zitakazofanyika jijini Mbeya.

“Wahitimu hao ni kutoka katika programu za uzamili, shahada ya kwanza, stashahada na astashahada,” alisema Prof. Kihanga.
Prof.Kihanga amesema maandalizi kwa sherehe hizo za kihistoria yameshakamilika ambapo, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta ndiyo atakaye watunuku shahada mbalimbali wahihitimu hao.

Mkuu huyo pia, amewaomba wakazi wa Mbeya na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi kwenye sherehe hizi za mahafali ambazo amezielezea kuwa zina maana kubwa sana katika tasnia ya elimu.

Idadi ya wanafunzi wa chuo hicho imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka kufikia wanafunzi 7,844 ilipofika June 2013, kutoka wanafunzi 1483 mwaka 2002/03, ikilinganishwa na wanachuo 7029 mwaka 2011/12.

“Mahafali haya ni ya pili kufanyika na yanafuatia yale yaliyofanyika katika kampasi kuu ya chuo hicho mjini Morogoro wiki iliyopita,” inasomeka taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chuo hicho, Bi. Rainfrida Ngatunga iliyotolewa jana.
“Chuo kimekuwa kwa zaidi ya asilimia 600 tokea kianzishwe mwaka 2002,” inasoma taarifa hiyo.

Bi. Ngatunga amesema  kuwa Kati ya wanafunzi waliopo, asilimia 45 ya wanachuo ni wanawake na asilimia 55 ni wanaume.
“Hii inafanya Chuo Kikuu Mzumbe kuwa na uwiano wa juu wa wanafunzi kijinsia kuliko vyuo vyote hapa Tanzania,” alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...