Akizungumza wakati wa maonyesho hayo katibu wa tawi ndg Hassan Kapilima alisema umefika wakati kila mtanzania, taasisi na vyama mbalimbali vya siasa kutangaza utamaduni wa Tanzania ili kuweka kumbukumbu sahihi na taswila ya mtanzania ndani na nje ya nchi.
KATIBU WA TAWI NDG HASSAN KAPILIMA
Mgeni rasmi katika maonyesho hayo alikuwa mwenyekiti wa tawi Ndg Salim Mfungahema, mwenyekiti alifurahishwa na maonyesho hayo ambayo yaliudhuriwa na watanzania na wasio watanzania, katika taarifa yake fupi alipendekeza kuwepo na utaratibu wa kutangaza nchi na utamaduni wetu mara kwa mara katika maazimisho mbalimbali kama kuzaliwa kwa CCM, sherehe za muungano, mapinduzi ya Zanzabar na sherehe za mwaka mpya, Mgeni rasmi ndg Mfungahema alisema kwa kufanya hivyo tutapata watalii wengi nchini na kuliingizia taifa fedha nyingi za kigeni na kukuza uchumi wa nchi.
Mwanautamaduni maarufu Moscow Bi Neema Mwambi akimpokea mwenyekiti wa tawi kwa furaha, mwenyekiti wa tawi Ndg mfungahema Salim alialikwa kuhudhuria maonyesho hayo.
Mwenyekiti wa tawi Ndg Salim Mfungahema (wa tatu kutoka kushoto mwenye shati la kijani)akiwa kwenye picha ya pamoja na watanzania na wasio watanzania kwenye maonyesho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika jijini Moscow-Urusi.


.jpg&container=blogger&gadget=a&rewriteMime=image/*)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...