Timu ya wachezaji wa zamani wa Tanzania, All Stars wameondoka leo kwenda Nairobi, Kenya kucheza mechi maalum ya kirafiki dhidi ya wachezaji wa zamani wa Kenya, Wazee wa Kazi   uliopangwa kufanyika kwenye uwanja wa Nyayo siku ya fainali ya michuano ya Chalenji.

Wachezaji hao waliondoka chini ya nyota wa zamani, Kitwana” Popat” Manara ambao walikuwa wakijifua kwenye uwanja wa Leaders Club kujiandaa na mechi hiyo.

Mbali ya Kitwana, wachezaji wengine ni Khalid Abeid, Omari Gumbo, David Mwakalebela, Lawrence Mwalusako, Mohamed “Mmachinga” Hussein, Thomas “Uncle Tom” Kipese na Idd Seleman.

Wengine ni Mahmoud Uledi, Ken Mkapa, Shaaban Katwila,  Maulid Kinapo, Abdallah Maulid, Ali Yusuph Tigana , Rashid  Idd Chama, Habib Kondo, Abdallah Kaburu, Idd Seleman, Naftali Goha na Bita John. Viongozi wa timu hiyo ni Hassan Mnyenye.

Alisema kuwa matarajio yao ni kushinda mechi hiyo kutokana na mazoezi mazuri waliyoyafanya chini ya kocha wao Talib Hilal.

Mchezo huo umepangwa kuanza saa 8.00 mchana kwenye uwanja wa Nyayo nan i moja ya kuongeza mashamsham ya fainali ya Chalenji na vile vile kuadhimisha siku ya Uhuru wa Kenya.

Wazee wa Kazi wapo katika mazoezi makali tayari kwa mchezo huo wa aina yake. Kikosi cha timu ya Wazee wa Kazi kinaundwa na wachezaji magwiji kama James Siang’a, Mohammed Abbas, John Busolo,Josphat Murila, Elly Adero, Sammy Pamzo Omollo, Thobias Jua Kali Ochola, Ben Oloo, George Onyango, Wycliffe Anyangu, Paul Ochieng na John Bobby Ogola.

Wengine ni Allan Thigo, Paul Onyiera, Joe Kadenge , Peter Dawo , Ben Musuku, Aggrey Lukoye, J.J Masiga , Mike Amwayi, Douglas Matual, Joe Birgen, Abdul Baraza, Ricky Solomon, James Nandwa, Ambrose Golden Boy Ayoyi, John Nyawaya, David Ochieng’ na Austin Oduor. Timu hiyo ipo chini ya kocha George Sunguti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. usisahau kutuwekea picha za wachezaji wetu wa zamani katika mechi hii , naona sunday manara hayumo kwenye list

    ReplyDelete
  2. Hata Malota Soma pia hayumo......Zamoyoni Mogella hayumo....ndio kusema wamechoka sana au vp?

    ReplyDelete
  3. Where is Peter Tino?Mzee Tenga nae avae jezi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...