Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya mwaka 2013 ambayo hutolewa kila mwaka na Shirika la Afya Duniani, Balozi aliwaeleza wageni waalikwa katika hafla hiyo kwamba ushiriki wa viongozi wa afrika kupitia mtandao wao wa ALMA umechangia sana katika kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na Malaria.
Dkt. Robert Newman kutoka WHO yeye amesema, inasikitisha pale inapobidi mtoto apoteze maisha kwa sababu tu ameshindwa kupatiwa chandarua ambayo thamani yake ni dola tano. amewataka viongozi na washirika mbalimbali kutobweteka na mafanikio katika kuudhibiti ugonjwa huo mafanikio nayohusu kupungua kwa maambukizo ya ugonjwa wa malaria na vifo vya watoto chini ya miaka mitano.
Bw, Ray Chambers ambaye ni Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema inatia moyo sana kuona vitanda katika wadi za watoto vikiwa vitupu mahali ambapo watoto walikuwa wakilala wawili katika kitanda kimoja kutokana na kusumbuliwa na malaria.
Dkt. Fatoumata Traore ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Roll Back Maralia akizungumza wakati wa halfa hiyo.
Katibu Mtendaji wa ALMA Bi. Joy Phumapi naye akizungumza machache.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Si wongo vyandarua vimesaidia. Sekta binafsi nchini nayo isaidie kusambaza vyandarua vijijini. Tusitegemee wafadhili tu.

    ReplyDelete
  2. Watanzania amkeni, kweli chandarua kinasaidia lakni kwa maoni yangu mimi nilikuwa naona bora ni kukomesha mazalio ya mbu kwa kunyunyiza dawa kwenye maji yaliyo tuwama na sehemu za mapori, hii itakua malari byebye vinginevyo tutakua ni sawa na kufua nguo kisha kunika kwenye tope.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...