Rais wa Marekani,Barack Obama akihutubia maelfu wa waombolezaji wa Msiba wa Rais wa Zamani wa Afrika Kusini,Hayati Nelson Mandela waliopo kwenye Uwanja wa FNB Soccer City,Jijini Johannesburg.Rais Obama amemsifia sana Mzee Mandela na kwa mengi aliyoyafanya kwa Waafrika Kusini na Dunia nzima kwa Ujumla.
Familia ya Hayati Nelson Mandela ikifuatilia misa maalum ya kumuombea kiongozi huyo Maarufu Duniani pamoja na kwamba mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.
Maelfu wa wananchi wa Afrika Kusini wakiwa wamefurika kwenye Uwanja wa FNB Soccer City,Jijini Johannesburg.
Rais wa Marekani,Barack Obama na Mkewe wakiwa kwenye misa hiyo.
Mke wa zamani wa Hayati Mzee Nelson Mandela, Winnie Madikizela-Mandela akionekana ni mwenye huzuni mkubwa wakati wa ibada maalum iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa FNB Soccer City,Jijini Johannesburg.
Mke wa zamani wa Hayati Mzee Nelson Mandela, Winnie Madikizela-Mandela akionekana ni mwenye huzuni mkubwa wakati wa ibada maalum iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa FNB Soccer City,Jijini Johannesburg.
Mke wa zamani wa Hayati Mzee Nelson Mandela, Winnie Madikizela-Mandela (kushoto) na mjane wa sasa wa Mzee Mandela,Mama Graca Machel ( kulia mwisho ) wakifuatilia misa hiyo.
Maelfu wa wananchi walijitokeza katika misa hiyo pamoja na mvua kubwa kunyesha muda mrefu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...