Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Kiwila,akipeleka mkungu wake ndizi ndani ya soko la Lembuka,mkoani Mbeya.
Sehemu ya mikungu ya ndizi ikiwa iko sokoni ikiuzwa ndani ya soko la Lembuka,Kiwila mkoani Mbeya.Kwa mujibu wa Wakulima wa zao hilo wanaeleza kuwa huu ni wakati wake wa kuvunwa kwa wingi,tatizo kubwa ni mfumo wa bei kuwa chini kutokana na kulanguliwa na wafanyabiashara wakubwa wanaonunua zao hilo kwa jumla na kusafirisha mikoa mingine kwa Malori.
Mkazi wa Kiwila,Mkoani Mbeya akipeleka mikungu yake ya ndizi kwenye soko la Lembuka,Kiwila wilayani Rungwe,mkoani Mbeya.Mkungu wa Ndizi huuzwa kwa bei kati ya shilingi 5000 mpaka 10,000/
Na hili ndilo tatizo kubwa linalotufanya sisi Waafrika na hasa Watanzania tuendelee kubakia masikini, mazao yetu hatuwezi kuyasindika thamani ikaongezeka, hebu cheki midizi yote hiyo, hata zingetengenezwa banana wine ikatiwa katika chupa mtu angeweza kuja kuuza akapata faida kuliko hiyo kuuza mkungu 5,000/-
ReplyDeleteHivi serikali za wilaya zina kazi gani kama masoko nayo yanasubiri wazungu waje kutuwekea mikakati ya mpangilio.Hivi kweli inaonyesha hakuna hata mmoja mwenye akili timamu kwenye huo mpangilio wa ndizi.waafrika tuna kazi sana.mpangilio hauhitaji pesa za kigeni hata kidogo sasa hap[o mnunuzi atapiata wapi kuchagua mkungu,Gosh
ReplyDeleteTafuteni maarifa ya kuoka banana bread!
ReplyDeleteKelele nyingi za nini..? Nendeni mkafanye sasa..sio kila kitu serikali..mmeshaona kunahaja ya kuinua soko hilo basi hamna budi kuanzisha kama ni usindikaji,uokaji wa bananna bread etc..tuache kelele nyingi na tuanze vitendo vingi
ReplyDelete