MWANASHERIA wa Mhe Zitto Zuberi Kabwe (Mb), Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, Ndugu Albert Msando, leo atazungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika Hoteli ya Serena kuanzia saa nne na nusu asubuhi (saa 4.30 asubuhi).
 
Dhima ya mkutano huu itakuwa kutoa ufafafunuzi juu  ya mashitaka 11 na majibu yake  ambayo Mhe. Zitto Kabwe  na washitakiwa wenzake walipewa na Kamati Kuu ya CHADEMA. Aidha, katika kikao hiki Ndugu Msando, kwa niaba ya wateja wake, ataeleza hatua ambazo wateja wake wanazichukua ndani ya chama katika kuhakikisha kwamba mgogoro uliopo unakwisha kwa amani na haraka iwezekanavyo bila kuleta athari zaidi kwa chama. 
 
Tunatanguliza shukrani na tunaomba waalikwa wazingatie muda.
 
Imetolewa na Ofisi ya Mbunge Zitto Kabwe,
Jumanne, 10 Desemba 2013
Dar es Salaam 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. KAMA KWELI NIA NI KUMALIZA MGOGORO KWA NI HAYA USIPELEKE NDANI YA CHAMA, KWA NINI UWAITE WAANDISHI WA HABARI ? SI UNATAKA WATU WACHANGIE NA HIVI KUKUZA AU KUCHOCHEA TOFAUTI.
    SIONI KAMA KUNA NIA YA KWELI YA KUTAKA KUMALIZA MGOGORO BAL NI KUONGEZA NA KUKUZA USHINDANI TU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...