Na Denis Mlowe.Aliyekuwa Arusha
WANANCHI  wa wanaozunguka   hifadhi   ya  Taifa ya Ziwa Manyara iliyoko mkoani Arusha wametakiwa kulinda hifadhi hiyo kwa kuachana na kulima katika vyanzo vya maji na maeneo yanayoizunguka hifadhi hiyo.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa TANAPA Dk.Ezekiel Dembe hivi karibuni wakati akizungumza na  wanahabari mkoa wa Iringa ambao  walikuwa katika ziara ya mafunzo ya kutangaza utalii katika  Hifadhi za Kaskazini.
Alisema kuna hatari kubwa ya  Ziwa Manyara kukauka zaidi kutokana na wananchi kuendelea kulima na kupelekea ziwa kujaa tope kutokana na kilimo hicho cha pembezoni.

Dk.Dembe alisema kutokana na kisichozingatia uhifadhi wa Ziwa Manyara baadhi ya ofisi za hifadhi  hiyo zimeharibika vibaya kutokana na mafuliko hivyo Tanapa wana mpango wa kutafuta  eneo  jingine ili kujenga ofisi  hizo.
Akizungumzia ubovu  wa  miundo  mbinu katika hifadhi za Taifa alisema kuwa  TANAPA  wapo katika mkakati kuboresha miundo mbinu  hiyo ili kuvutia  zaidi watalii wanaofika katika  hifadhi  hizo kuendelea kupitika kwa urahisi kwa mwaka


Akielezea kuhusu hifadhi ya Taifa Ruaha iliyoko Iringa kutangazwa kama ilivyo hifadhi za Kaskazini Dk. Dembe, alisema kuwa hivi  sasa mkakati umewekwa wa kuelekeza nguvu ya kuitangaza hifadhi hiyo  ili kuvutia watalii  zaidi  japo alisema  changamoto  kubwa ni upatikanaji wa mafuta  ya Ndege ambazo zinaleta  watalii ambao  hulazimika kujaza mafuta Dodoma .
“Hata  hivyotumeanza mkakati wa kuhakikisha hifadhi ya Katavi na Ruaha katika viwanja wa ndege  vilivyopo  huko kunakuwa na mafuta ya ndege  kupunguza gharama ambazo watalii wanatumia kwa sasa” alisema Dk. Dembe 
Alisema TANAPA wako katika mchakato wa kutafuta  wawekezaji wa kujenga  Hotel za kisasa katika hifadhi ya Ruaha ili kuvutia  watalii wengi zaidi.
Kuhusu  usalama wa watalii alisema kuwa  TANAPA wamejipanga  kuweka usalama mzuri wa watalii ili ni pamoja na kuanzisha ulinzi wa askari  watakaofanya kazi ya kulinda  watalii pekee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...