Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu(kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuchezesha droo kubwa ya mwezi ya Promosheni ya “Timka na BodaBoda”kulia ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Humudi Abdulhussein,Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

Watanzania washauriwa kuchangamkia Promosheni ya Timka na Bodaboda,kwani zimebaki siku 44 tu zinazoweza kubadilisha maisha yao kabisa na kuwa mazuri na yenye maendeleo.

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambayo ndiyo inaendesha zoezi hilo imetoa wito huo kupitia Meneja Uhusiano wa Umma na kuweza kutangaza kwamba mpaka sasa jumla ya washindi 230 wamejishindia pikipiki maarufu”Bodaboda” na jumla ya fedha taslimu kiasi cha shilingi Milioni 142 zikiwa tayari zimekwisha tolewa ambapo Milioni moja moja zilikwenda kwa washindi 92, Milioni 5 zikienda kwa washindi 8, wakati mjasiriamali mwanamama, ambaye ni mkazi wa Arusha,Haika Mosha akiibuka kinara wa mwezi na kujishindia kitita cha shilingi Milioni 10.

Akizungumzia kuhusiana na promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu alisema “mwitikio umekuwa mkubwa sana tangu wamezindua promosheni hiyo mpaka hapa tulipofikia kwani watu wamekuwa wakijishindia bodaboda kwa ajili ya usafiri ama kuanzisha biashara na pia fedha taslimu ambazo zimekuwa zikitumika kufanyia biashara ama kuongeza mitaji yao na matumizi mengine ya kimaisha.”

“Promosheni hii inamlenga kila mwananchi kwani tatizo la usafiri ni letu sote na pia kilio cha watu kutokuwa na fedha za kukuza au kuongeza mitaji yao ya kibiashara ni sugu kwa kila Mwananchi. Hivyo basi kwa hali niliyoiona kwamba mitaji ni kilio kikubwa cha wajasiriamali wengi nchini,kwa kuunga mkono jitihada za wajasiriamali nchini Vodacom ndiyo maana tumekuja na promosheni hii,Hivyo tunaamini kupitia promosheni hii ya kuwafanya wateja wetu kushinda bodaboda pamoja na fedha hizi tunazozitoa kwa washindi zitasaidia kupiga hatua na kuweza kubadilisha maisha ya watanzania.

Pia napenda kuwaasa washindi wote wa promosheni hii kutumia pesa zao ipasavyo kwa kuwekeza katika masuala ya kimaendeleo na kuleta manufaa katika jamii inayowazunguka.Alisema Nkurlu.Ili kujiunga na promosheni hii wateja wanatakiwa kutuma neno PROMO kwenda 15544.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...