Katika kuimarisha umoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuonyesha kwa vitendo Upendo na ushirikiano wa asilia uliopo tangu enzi za mababu zetu katika wana Afrika Mashariki kabla ya mkoloni na kuelekea kuwa na sarafu moja hatimaye shirikisho, Luton Tanzanian Community (LTC) Uingereza Kwa mara nyingine tena kwa kushirikiana na Tripple EM Inawaletea Sherehe za Uhuru wa Tanzania na Kenya (Double Celebrations ) Jumamosi Tarehe 14/12/2013, Roman Way Tomlinson Avenue LU4 0QL - Luton.

Kutakuwa na burudani za kumwaga vichekesho na majonjo ya asilia yetu wana East African; Nyama Choma, Tusker, Safari na Vyakula asilia vya nyumbani km. Ugali, Kienyeji, Mihogo ya Kuchoma chachandu, Chapatti original za east afrika, Samaki n.k Kiingilio ni Paundi tano tu (£5) kabla ya saa sita usiku na baada ya hapo ni Paundi kumi (£10).

Magoma yote ya mwambao , bongo flava za aina zote, pia kutakuwa magoma toka pande zote za wana jumuiya wa Afrika Mashariki King James Narashize music toka Rwanda , Big Fizzo BAJOU Fariouz" Burundi music, Chamelion music toka Uganda , DNA toka Kenya, na Mayenu kama kawa chini ya ma DJs CYMOH, DJs PAPS, DJs JOE HAMEL na Mtaalam DJs Double T wataangusha magoma kuanzia saa mbili usiku mpaka Majogoo Pia kutakuwa na suprises kubwa za kutisha siku hiyo usikose Watanzania na Wakenya watasindikizwa na wenzao toka Uganda, Burundi na Rwanda katika kuimarisha ushirikiano wa wana Afrika mashariki pia kutakuwepo na marafiki wa Afrika Mashariki hapa UK.

Wote Mnakaribishwa:

Abraham Sangiwa
Katibu - Luton Tanzanian Community - Uingereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Tunataka Afrika ya Mashariki ya namna hii!

    Sio Afrika ya Mashariki ya 'Coalitionof the Willing'-CoW.

    Tukumbuke Wakuu wetu waliotangulia kama Mzee Madiba aliyeanguka wiki iliyopita huko Kusini ambaye Msiba ndio mbichi tunao, akina Nyerere, Kwame Nkumah, Jomo Kenyatta,Lumumba na wengineo walipenda Utangamano na Muungano na sio Utengano!!!

    Mungu Ibariki Afrika ya Mashariki!

    ReplyDelete
  2. sasa hapa mambo yanawiva wana afrika mashariki sisi ndiyo wenye sauti ya umoja wetu tusikubali kubomoa umoja wetu wa kiasili na wenye manufaa kwetu sote "big up" Luton Tanzanian Community kwa kutuunganisha pamoja mpaka huku ughaibuni, na ujumbe ufike EA kwani tunaona manufaa ya wenzetu huku na European Union yao tuna mengi ya kujifunza toka kwa wana EA Waliopata exposure toka EU countries. Idumu Jumuiya ya Afrika Mashariki.

    ReplyDelete
  3. Hii ni habari njema ya ushirikano na majirani zetu.

    ReplyDelete
  4. The mdudu, anasema kwa unafiki wa hao mikenya mm siji hata kwa fimbo,na huu ujumbe uwafikieni nyie watanzania njaa mnao andaa hii sherehe kwa kuangalia matumbo yenu pasipo kufuata misingi halisi ya Uhuru wetu kama watanzania halisi acheni kujipendekeza na huo muungano mbona hao wanafiki wenzenu wakiwa na sherehe zao hawatuiti? Amakweli njaa mbaya sn ndugu zangu watanzania mlioko huko nyumbani muwe makini na watanzania kama hawa wanojipendekeza kwa mijitu ambayo haitupendi kabisa,watu kama hawa huku wako kuangalia matumbo yaoo tu,

    ReplyDelete
  5. Mchangiaji wa nne umeongea ukweli, kuna ambao watakupinga pasipo fanya utafiti ila huo ndio ukweli wenyewe jamaa hawako kiurafiki na watz sijui kwa waganda ila jamaa sio tunawaona hata huku nyumbani kwenye taasisi au mashirika na kampuni walizopo jinsi wanavyojiona wako juu lakini ukija kwenye vitendo wako nyuma sana hawawawezi watz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...