MWANASHERIA Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema  (pichani kulia) amesema

wanashughulikia kisheria suala la Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Kabwe  (pichani chini) kudanganya bunge na kamati kuhusu majina ya watu walioficha mabilioni ya fedha Uswisi. 
Jaji Werema, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya kuchunguza madai ya mabilioni hayo amesema ili kumalizia uchunguzi wa fedha hizo ameomba Naibu Spika wa bunge kuongezea kamati hiyo miezi sita. 
Akitoa majumuisho ya taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Kamati ya Bunge ya Katiba ,sheria na Utawala , Jaji Werema alisema alishangaa kitendo cha Mhe. Zitto kutaka suala hilo liangalie mfumo na siyo majina ya watu walioficha mabilioni hayo. 
Jaji Werema alisema awali yeye alishauri kuangalia mfumo wa uwekaji wa fedha hizo lakini Mhe. Zitto alikataa na kusema anataka kutoa dukuduku kwa kutaja majina ya watu walioficha hizo. 
Alisema mwezi Februari kamati ilikutana na Mhe. Zitto na kuwaeleza kuwa ana taarifa na nyaraka na kutoa masharti lakini aliondoka ka kwenda katika kambi ya jeshi kwa mafunzo ambako kamati ilimfuata lakini bado aliwataka kukutana Dar.
Alisema Mei mwaka huu amekuwa akiichenga kamati hiyo hadi Oktoba ndipo alipokiri kwa kiapo maalum kuwa hakuwa na jina wala akaunti ya mtu yeyote ambaye ana fedha nchini Uswizi. 
“Jambo la kushangaza ni leo kudai serikali haina dhamira na suala la walioficha fedha uswis?kwa kweli  Mhe. Zitto Kabwe ni mzigo na sasa tunaingia kufanya kazi hiyo ya uchunguzi kama serikali kwa kutafuta taarifa bila kumuonea mtu”alisema  Jaji Werema .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. teh.. teh.... mmeona eeh. huyo ni tatizo!!!mbona hata yeye ameficha za kwake zinakuja kwa western union!1

    ReplyDelete
  2. Huu si wakati wa kukashifiana lazima watu watumie hekima, ikiwa kweli Mh. Zitto anayo majina hayo na akayatoa ni kujitafutia hatima yake ya kisiasa na hata kimaisha. Ikiwa kweli kuna watu wana mapesa nje ya nchi ni bora wawekeze nchini ili na wananchi nao wafaidike!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...