![]() |
Katibnu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue |
Na Kiza Sungura
- MAELEZO
KATIBU Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ameitakaTimu ya Wataalamu 14 Wazalendo wa Mkataba wa Maliasili wa Tanzania kutekeleza majukumu yao kwa makini kwa sababu mkataba huo unazingatia maslahi makubwa kwa nchi yao.
Balozi Sefue ametoa wito huo jijini Da es Salaam wakati akizindua timu hiyo yenye jukumu la kutoa ushauri na elimu wa kitaalamu jinsi Tanzania itakavyonufaika na rasilimali zake.
Alisema katika kutekeleza majukumu yao wahakikishe kuwa wanachukua kila maoni mazuri yatakayowasilishwa kwao na kuhakikisha kwamba yanaifikisha nchi katika kutumia vyema maliasili zake.
“Jambo la pili nawataka muweke mbele maslahi ya taifa kwanza, si kwa maslahi ya taasisi mnazotoka.Mnatoka Serikalini, Sekta Binafsi, Taasisi za Elimu na Asasi za Kiraia, lakini kwa jukumu hili kuweni wazi na msifungwe na nafasi mlizonazo.Iwekeni Tanzania kwanza” alisema Balozi Sefue.
Aliwataka kwa pamoja kuchukua sekta ya gesi na maliasili nyingine nchini na kuzifanya kuwa neema na sio ziwekiza, majuto na kusababisha kupotea kwa utulivu wa nchi.
Timu hiyo inayoundwa na wataalamu 14 na wengine wawili ambao watateuliwa baadae, inaongozwa na Profesa Florens Luoga kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wajumbe ni Judith Kairuki kutoka Kituo cha UwekezajiTanzania(TIC).
Wengine ni Mhandisi Nobert Kahyoza kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Charles Mwapinga kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Gabriel Bujulu kutoka Shirika la Maendeleo ya Peotroli Tanzania (TPDC), Dk. Fidea Mgina kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Wataalamu wengine wanaounda timu hiyo ni Athumani Kwariko kutoka Tanzania Extractive Industreis Transparency International (TEITI), Ignace Mchallo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Siraji Majura kutoka Wizara ya Fedha na Uchumi,
Godwin NyelokutokaTaasisiya Tanzania Chambers of Minerals and Energy, John Ulanga kutoka Taasisi ya Asasi za Kiraia.
Wengine ni Deo Mwanyika kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Yonika Ngaga kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Profesa Hamudi Ismail Majamba kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
The mdudu,anasema is back again coz karilazwa baada ya kupatwa na msituko wa moyo,baada ya kusikia ile habari ya Tajiri mmoja anae miliki eneo la machimbo ya DHAHABU lenye ukubwa wa zaidi ya mkoa wa DAR,,tukija kwenye mada ya hao WASOMI walioteuliwa na kuambiwa waiweke TANZANIA KWANZA,chonde chonde nyie wasomi kafanyeni mlicho tumwa ili muikoe nchi kimaendeleo jiepusheni kabisa na vishawishi vya aina yoyote ile, haya ni hayo tu kwa leo, maana hapa nilipo taabani moyo moyo ndugu zangu watanzania,msiombe mkakutwa na ugonjwa wa moyo ni hatari sn,
ReplyDeleteMh.Katibu mkuu mtemdaji!
ReplyDeleteNashukuru kwa utewndaji wako mzuri wa kazi chini ya Jenerali Jakaya Kikwete,lakini nataka kuuliza swali moja tu. Lini mtatuletea Balozi katika kanda ya RUSSIA na nchi zilizo chini ya himaya hiyo nikizingatia kuwa RUSSIA na nchi zinazosimawiwa na Balozi huyo ni kubwa sana na inaweza linganishwa tu na MAREKANI. Hivyo tafadhali jitahidini maana ni kama miezi minane tumeakaa bila Balozi baada ya Balozi Jaka Mwambi kumaliza mda wake hapo April mwaka huu.
Nauhakia hili utamfikishia Bwana mkubwa JK afanye uamuzi mapema.
Ndugu yangu annony na2. Maoni yako ni mazuri, lakini kwa jinsi tulivyowaona ndugu zako huko Urusi na marafiki zao wameonyesha tabia za ubaguzi za kutokuja na kuungana na dunia yote katika kupinga na kulaani ubaguzi duniani na kumpongeza shujaa wetu wa upinzani wa Ubaguzi huo duniani Nelson "Madiba" Mandela. Hao tunawafananisha sawa na walivyo katika ubaguzi wao weusi wenzetu Wa Nyarwanda. Hawakuja kulaani kitendo cha ubaguzi kama alivyofanya Nelson Mandela kama walivyofanya Warundi. Wanyarwanda hawa eti tunategemea tuwe nao katika Jumuia Ya Afrika Mashariki ni kweli tunawahitaji kweli? Mbona ni wabaguzi kiasi hicho?. Lol shame on them. - Mr MHOJA - Sweden
ReplyDelete