Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Allan kijazi akiwahutubia wahitimu wa mafunzo ya kuhifadhi maliasili katika chuo cha wanyama pori cha Mlele mkoani katavi ambao hawapo pichani hapo juzi katika chuo cha wanyama pori cha mlele ambapo wahitimu 96 walihitimu mafunzo ya awali ya wahifadhi wa rasilimali za nchi na aliwataka wafanye kazi kwa uadilifu mkubwa ili waweze kupambana na kutokomeza ujangiri na kuvunja mitandao ya majangiri ya ndani ya nchi na nje ya nchi.
Askari wa hifadhi ya mbuga ya wanyama (TANAPA) wakiwa wamesimama wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA ambaye hayuko pichani wakati akifunga mafunzo ya askari hao waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika chuo wanyama pori cha Mlele mkoa wa katavi namna ya kulinda rasilimali za nchi ambapo amewataka wahitimu hao wafanye kazi kwa uaminifu
Askari wa hifadhi ya mbuga ya wanyama (TANAPA) wakiwa wamekaa wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA ALLAN KIJAZI ambaye hayuko pichani wakati akifunga mafunzo ya askari hao waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika chuo wanyama pori cha Mlele mkoa wa katavi namna ya kulinda rasilimali za nchi ambapo amewataka wahitimu hao wafanye kazi kwa uaminifu. Picha na Katavi yetu Blog.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...