Rais wa Jamhuri ya Sudan Mhe. Omar Al-Bashir, akiangalia Hati za utambulisho mara tu baada ya kuzipokea kutoka kwa Balozi Dkt. Batilda Salha Buriani katika Ikulu ya Khartoum.
Mhe. Rais Omar Al-Bashir akipeana mkono na Mhe. Balozi Batilda muda mfupi kabla ya kupokea rasmi Hati za utambulisho kutoka kwa Mhe. Balozi kwenye ofisi za Ikulu ya Sudan
Mhe. Balozi akimtambulisha ndg. Nicholaus J. Mwakasege, afisa wa ubalozi wa Tanzania Nairobi kwa Mhe. Rais Omar Al-Bushir
Mhe. Omar Al- Bashir akifanya Mazungumzo na Mhe. Balozi Batilda kwenye Ikulu ya Rais wa Sudan
Mhe. Balozi Batilda akikagua Gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake kwenye viwanja vya Ikulu ya Sudan
Mhe. Balozi Batilda akiwa amesimama na Maofisa wa serikali ya Sudan wakati nyimbo za Taifa za Tanzania na Sudan zikiimbwa na bendi maalum kwenye viwanja vya Ikulu, Sudan. |
Mhe. Balozi Batilda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Tanzania walioko SUdan.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...