Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula, akizungumza na uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dar es Salaam, kuwataka NSSF kufungua Ofisi zitakazotoa huduma za Westadi nchini Marekani ambazo zitawasaidia watanzania waishio nje ya nchi kusafirisha mwili wa marehemu pamoja na kupata huduma ya matibabu kwa ndugu wanne waliopo nchini. Kushoto ni Kaimu Meneja Kiongozi na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Theopista Muheta. 
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula (kulia), akizungumza na uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dar es Salaam, kuwataka NSSF kufungua Ofisi zitakazotoa huduma za Westadi ambayo itawasaidia watanzania waishio nje ya nchi kusafirisha mwili wa marehemu ikiwemo huduma ya matibabu kwa ndugu wanne waliopo nchini. Kushoto niKaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matessa.   
 Ofisa Mwandamizi wa huduma za Westadi, Boniface Kanemba akifafanua jambo wakati wa mkutano huo. 
 Maofisa wa NSSF wakiwa katika mkutano huo.
 Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu (kulia),   Ofisa wa NSSF, Neila Kambaya na  Halima Mgala.
Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji wa NSSF, Abdalah Mseli akizungumza katika mkutano huo. 
 Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja 
 Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Westadi. 
 Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matessa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mimi ni mteja wa NSSF katika WESTADI. Mmoja wa wadau wa kwanz katika hili. Nilipotoa wazo la wao kuwa na mwakilishi na hata kujitangaza kwa mmoja ya viongozi wa NSSF nilijibiwa, "hakuna sababu, kwani hao watu hawajui umuhimu?" Kwa kweli nilishangazwa na kiwango cha ujinga wa kiongozi mkubwa wa taasisi kama hiyo. Kazi tunayo Tanzania.

    ReplyDelete
  2. njie watanzania huko Marekani na Ulaya na mkate bima za mazishi na kurudisha miili yetu nyumbani mtakapokufa. Tumechoka na kuombwa michango michango. mdau AlexBura dar.

    ReplyDelete
  3. Hatuhitaji ofisi marekani, application tunafanya online na malipo pia. Hizo hela za kufungua ofisi zitumike kufanya maendeleo hapo Tanzania sio kuchezea hela.

    ReplyDelete
  4. Mdau hapo juu hujaombwa kuchangia hizo pesa. Temea mate chini. Kufunguliwa ofisi nakubaliana nalo 100 percent. They just need to recruit someone huku USA wako wengi. Imagine mikoa 50 yote ni wangapi?

    ReplyDelete
  5. Idara ya information technology kichefuchefu. Nilikua naweza kuangalia statement zangu online ghafla haikubali. Nime submit query online huu mwezi wa 6 no one bothered to reply hata kama hana solution. Leo wanapeleka product nje ya nchi sijui itakuaje? Nssf ni taasis kubwa, inasikitisha hawana hata tamaduni ya ku address complaints kwa wakati

    ReplyDelete
  6. Problem sio NSSF peke yake kuna watu wanaitwa CRDB walikuja kwa mbwembwe wakatujazisha form tangu kipindi kile JK kaja US hadi leo hakuna kilichofanyika, ukituma email hata kwa Wakurugenzi wao hayo majibu yao unachoka kabisa sasa huku wanakujaga kufanya nini shopping au kutusaidia? Na Kwanini hawajibu wateja? Kwenda sambamba na dunia ya leo mambo ya online iwe banking ama any transactions lazma mjirekebishe

    ReplyDelete
  7. kaaaaaaaazi kweli kweli.......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...