Sarafu ya thamani ya sh 50,000 iliyotengenezwa kwa madini ya fedha kwa asilimia 92.50
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Benno Ndulu
---
 BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa sarafu maalumu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye thamani ya sh 50,000. Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, amesema kuwa sarafu hiyo iliyotengenezwa kwa madini ya fedha kwa asilimia 92.50, imetolewa kwa ajili ya kumbukumbu tu na haitaingizwa katika mzunguko wala kutumika kwa kulipia malipo ya aina yoyote.
 Sarafu hii imetolewa maalumu kama maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar, haitatumika kwa manunuzi. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya BoT ilimnukuu Profesa Ndulu akisema sarafu hiyo imetolewa kwa idadi ya vipande 3,000 kwa ajili ya tukio hilo na kuwahimiza wananchi kuinunua kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.
Kwa mujibu wa Gavana Ndulu, kutolewa kwa sarafu hiyo kunakwenda sambamba na utaratibu wa Benki Kuu kutoa sarafu maalumu za aina hiyo kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya matukio mbalimbali muhimu ya kitaifa na kimataifa.
“Kwa kawaida, baada ya muda, thamani ya sarafu kama hizi huongezeka na kuwa na faida zaidi kwa wanaozimiliki,” alisema Profesa Ndulu.
Gavana Ndulu alieleza sarafu hizo zitapatikana Januari 5 kwa bei ya sh 50,000 katika matawi ya benki za biashara zitakazokuwa zimepata sarafu hizo kutoka Makao Makuu ya Benki Kuu, Dar es Salaam na matawi ya Benki Kuu yaliyoko Zanzibar, Arusha, Mbeya na Mwanza.
“Benki za biashara zinaweza pia zikasambaza sarafu hizi kupitia matawi yake,” alisema gavana na kuongeza taarifa za usambazaji zitatolewa na benki hizo.
Katika sarafu hiyo, upande wa mbele unaonyesha sura ya hayati Sheikh Abeid Aman Karume na maandishi yanayosomeka: ‘Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi’.
Upande mwingine wa sarafu unaonyesha nembo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, maandishi yanayosomeka: “Miaka Hamsini ya Mapinduzi”, thamani ya sarafu na miaka 1964-2014.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Ama kweli maisha ya sasa ni kama walivyo sema ya kuwa LAKI SI PESA!

    Yaani ukiwa na Sarafu mbili sio Mia Mbili bali ni LAKI MOJA.

    Prof.Ndulu au sio?

    ReplyDelete
  2. Prof. Ndulu,

    Hiyo sio Currency demutualization?

    Yaani kuishusha thamani Shilingi?

    ReplyDelete
  3. Prof. Ndulu,

    Ewe bwana Mapesa BoT kwa kutoa Sarafu mpya ya 50,000/= mbona umetukwamisha hivi Waoaji?

    Siku zile ilikuwa ukienda Kijijini na hata ukitoa Mahari ya ELFU AROBAINI lakini ya (NOTI NYEKUNDU ZA MSIMBAZI 4 ZA 10,000/= KILA MOJA) unapewa mke!

    Sasa tutawabeba vipi Wazee wa Vijijini kuwapelekea hata kama ni SARAFU MOJA YA ELFU HAMSINI si tutawajibishwa Ukweni na wazee kwa kuleta dharau ?

    ReplyDelete
  4. Ohhh Prof. Ndulu,

    Hivi kwa hali ya Uchumi wa Magu, Kwimba na Malampaka huko vijijini si ndio Sarafu mpya ya 50,000/= itachochea Kupanda kwa gharama za maisha na Mfumuko wa bei?

    ReplyDelete
  5. Wote mliochangia hapo juu kasomeni tena maelezo ya gavana. Naona hamjaelewa

    ReplyDelete
  6. someni maelezo ndio mtoe maoni

    ReplyDelete
  7. someni maelezo ndio mtoe maoni

    ReplyDelete
  8. ni meamini kuna watu hawapo kujadili wapo kwa ajili kulaumu na mabishano mbona maelezo yapo clear si kwa matumizi.....mnahitaji kurudi shule

    ReplyDelete
  9. Duuu ama kweli Prof. Ndulu ametutishia mnyau !!!

    Kumbe Sarafu hizo hazitakuwa ktk mzunguko wa fedha.

    ReplyDelete
  10. Gavana Prof. Ndulu na timu yake BoT wamefanya utafiti wametambua Watanzania wengi hamtumii kuweka fedha ktk Mabenki mnahifadhi fedha chini ya magodoro mnayolalia na sasa amefyatua Sarafu za 50,000/= ili mnunue na kuipeleka fedha Benki ninyi wenyewe!!!

    ReplyDelete
  11. Mimi nitakunya kahawa kikombe kimoja cha Shs. 50/= Kijiweni halafu wakati wa kutoa malipo nitachomoa Sarafu ya Elfu Hamsini!

    ReplyDelete
  12. ukitaka kujua watu wanakurupuka hawasomi kilichoandikwa..duuu nimekubali kweli kabisa huku kwetu tuwekee maarifa ya kupata pesa kwa maandishi uone kama kuna mtu atapata..hahahhah. kusoma c utamaduni wetu..hapo mtu kasoma kichwa cha habari tu.

    ReplyDelete
  13. Mimi nitakunya kahawa kikombe kimoja cha Shs. 50/= Kijiweni halafu wakati wa kutoa malipo nitachomoa Sarafu ya Elfu Hamsini!

    ReplyDelete
  14. The mdudu,ndugu zangu watanzania hii ndio nafasi pekee ya kuitumia na kuwakemea hao watu wa BANK KUU tuliowaamini kwenye sehemu nyeti kama hiyo,angalizo kwa wadau wote ikumbukwe mtu kama huyu ni nadra sn kuwapata hapa kwa mjomba MICHUZI leo kaja LIVE lakini MSG zenu zote utumbo mtupu,,ni nn cha kuwakemea na kustop kabisa ni MATUMIZI YA DOLA pesa ya U.S.A maana imeiteka pesa yetu ya SHILINGI ndio maana unakuta toka enzi na enzi pesa yetu imedumaa kama maji kwenye dimbwi ni kina nani hasa wanao coz pesa yetu ionekane silolote sichochote ni hawa hapa WAFANYABIASHARA WAKUBWA ndio wasioitakia mema pesa yetu,,nahuku serikali na wanasiasa wakilifumbia macho,ila LIPUMBA PEKEE NDIE anaelikemea hilo swala hongera sn kwake toka kwangu,mm niko mbali ila mambo muhimu kama haya huwa nayafuatilia sn sn coz inaniuuma moyoni kuona pesa yetu inakua HOI kila mwaka.mjomba nakuomba usiifiche plz cozi natoa yalio moyoni kwa wadau wenzangu ili tuikoe pesa yetu,

    ReplyDelete
  15. Niliishasema watanzania wengi mnoi uelewa ni zero! amini msiamini kama wadau hapo juu walivyosema kasomeni tena kabla ya ku-comment! hili ni tatizo sugu, ngoj EAC ianze muone wakenya na waganda watakabyochukua kazi zetu, then tunaishia kulalamika tu. Mungu iponye Tanzania na watu wake.

    ReplyDelete
  16. The mdudu,ww mdau unaesema sisi ni zero sikweli ila ww ndio 0,coz huoni mbali yaani hata hujui ya kwamba kuna katiba yetu ya Tanganyika inakuja? Sasa why unasema Mikenya na Miganda itachuka kazi zetu kwenye hiyo katiba yetu for sure hatuwezi kuluhusu ujinga kama huo,,na sio hao tu hata ndugu zetu wakutoka zanzibar waliokua wakiupinga muungano pasipo na kuona mbali matokeo yake ndio haya hasa hasa wazanzibar waliokua huku bara wajiandae na haya maswala kwanza kabra ya kutunga katiba yetu ya Tanganyika waludi wote zanzibar ili watupishe na kutupa muda wa kuitunga katiba yetu na ikiwa tayari tushaipata tuna wakaribisha tena ila kwa masharti haya,,1 mmepoteza kila kilicho chenu kwa hiyo mnaanza na moja coz katika katiba yetu mpya tumeweka vipengere ambavyo hamluhusiwi tena kumiliki ARDHI YA Tanganyika so vitu vyenu vyote vimetaifishwa je ndugu zangu WAZANZIBAR mshajiandaa na hilo? Na je nani atakua ameathilika zaidi ni sisi wakutanga muungano au nyie wa kuukataa muungano? Amakweli hakili nywele,mjomba nakuomba hili swala tulitafutie HOJA YA HAJA inayosema,,INAYOSEMA KWANINI WA BARA HAWARUHUSIWI KUMILIKI ARDHI ZANZIBAR? ILI HALI WAO WANAMILIKI ARDHI HUKU BARA? Mjomba nakuomba usiifiche hii ili itambaeeee kwa wadau wote.

    ReplyDelete
  17. Una chuki na roho ya fisi! Kwani Wazanzibari wakitoka wote utaweza jenga na upate utajiri bila kujituma?wazungu,wachina,wakongo na makabila yote wako Tanganyika,ila halijazuia wanao nia ya kufanya Nazi kufanikiwa.!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...