Makamanda na Wapiganaji wa Jeshi la Magereza wakiwa katika sherehe ya kuukaribisha Mwaka mpya wa 2014 usiku wa kuamkia leo katika Viwanja vya Bustani ya Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam
Maofisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakipita mbele ya Mgeni rasmi kwa ajili ya kutosti glasi za vinywaji katika Sherehe ya kuukaribisha Mwaka mpya wa 2014.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimpongeza mmoja wa Maofisa wa Jeshi la Magereza, Stafu Sajin Luckson Mtenga ambaye amezawadiwa zawadi ya Kipoza joto kutokana na kutenda kazi zake kwa kujituma na kuonesha nidhamu kiutendaji kwa Mwaka uliopita wa 2013.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa hotuba fupi kwa Maofisa wa Jeshi la Magereza (hawapo pichani) katika sherehe za kuaga Mwaka 2013 na kuukaribisha Mwaka mpya wa 2014. Sherehe hizo zimefanyika usiku wa kuamkia leo katika Viwanja vya Bustani ya Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam. Picha na Inspekta Lucas Mboje


.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...