Bondia Fransis Miyeyusho akihojiwa na waandishi wa habari huku akiwa amezungukwa na mashabiki wake mara baada ya kumtandika Bondia Joshua Amukulu kutoka nchini Kenya kwa Knockout (KO) raundi ya pili ya mchezo,wakati wa mpambano wao wa kufunga mwaka na kukaribisha mwaka mpya wa 201, uliofanyika katika Ukumbi wa Msasani Klabu,jijini Dar es salaam.
Bondia Fransis Miyeyusho akitunisha msuli wake kuonyesha umwamba alionao katika mchezo wa masumbwi.
Bondia Fransis Miyeyusho akimsukumia makonde mazito mpinzani wake,Bondia Joshua Amukulu kutoka nchini Kenya katika mpambano wao wa kufunga mwaka 2013 na kukaribisha mwaka mpya wa 2014, uliofanyika katika Ukumbi wa Msasani Klabu,jijini Dar es salaam.Miyeyusho alishinda kwa Knockout (KO) raundi ya pili ya mchezo.
Mpambano ukiendelea.
Bondia Fransis Miyeyusho (kushoto) akimsikilizia mpinzani kama kama ataendelea na mpambano mara baada ya kuanguk chini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hongera miyeyusho kwa kumaliza mwaka kwa ushibdu

    ReplyDelete
  2. Huu si mchezo. Ni uharibu wa ubongo wa binadamu. Inabidi ufutwe. Hapa Sweden mchezo huu hauruhusiwi

    ReplyDelete
  3. huu ni mchezo kama mchezo mwingine sema ukiutizama kijuujuu unaonekana kama ni mchezo wa hatarai sana. SIVYO UNAVYOFIKIRIWA.
    KINGINE MDAU HAPO JUU NI MUONGO MCHEZO HUU UNACHEZWA SANA HAPO SWEDEN NI WAO WAPO JUU ZAIDI YETU KINGUMI, MIMI MWENYEWE NIMESHAWAHI KUPIGANA STOCKHOM NA NIMESHAWASINDIKIZA MABONDIA TOFAUTI KUJA KUPIGANA SWEDEN AKIWEMO JOSEPH MARWA.
    MDAU TAFADHALI UONGEE KITU AMBACHO UNAKIJUA NA UNA UHAKIKA NACHO VINGINEVYO NYAMAZA. KAMA WEWE HAUPENDI WENGINE WANAUPENDA SANA

    ReplyDelete
  4. Pamoja na yote haya lakini mabondia wetu woooote wakikanyaga russia tu chali tena kwa KO.....nadhani wanapaswa kujifua zaidi, wasibweteke na huu ushindi unaotoka kwa hawa mabondia wasiojiweza wa hizi kanda zetu si mifano bora ya kujitathmini.

    ReplyDelete
  5. Huyu Bondia wa Kenya njaa kali. Mwili umechoka.

    ReplyDelete
  6. Hahahaha ,Mdau wa 5 hapo juu naungana nawewe.

    Cheka amecheza na Mgomba!

    Huyu Bondia wa Kenya amekuja tafuta Kazi za Uweita Mahotelini Tanzania wala sio Bondia kiukweli!

    Mnabisha?,,nendeni Mahoteli ya Masaki wiki ijayo mtamkuta amevua Gloves anakoti refu na kizibao anahudumia chai Hotelini!!!

    ReplyDelete
  7. Mdau wa 4 Russia Mabondia wanatumia sana Dopping (yaani madawa ya kuongeza nguvu) sio msuli wa kiukweli ndio maana wanawapiga sana wageni wakifika kwao!

    Hebu jiulize ni kwa nini Russia huwapigwa Mabondia wa nje wakiwa kwao, na Wa-Russia wakipigania nje ya Russia wanapigwa?

    Mabondia wa Kiukweli wasiotumia madawa ni wa Cuba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...