Gari ndogo aina ya Toyota Corolla lenye nambari za Usajili T 379 AGL,likiwa ndani ya Mtaro mara baada ya kupoteza mwelekeo likiwa kwenye Mwendo mkali.Tukio hilo limetokea mchana huu katika Barabara ya Migombani kama unaelekea Makao Makuu ya Kampuni ya simu za Mikononi ya Zantel.Ndani ya Gari hii kulikuwa na watu watatu ambao majina yao hayakuweza kufahamika kwa haraka kutokana hali iliyokuwa,wawili kati yao wameumia vibaya na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa,Gari hiyo ilionekana ikiwa kwenye mwendo kasi hali iliyopelekea kushindwa maarifa kwa dereva wakati akipishana na Bajaj.
 Wasamalia wema wakihangaina namna ya kumuokoa mmoja wa majeruhi kwenye ajali hiyo,ambaye alikuwa amenasa kutokana na kubanwa na sehemu ya Gari hilo.
 Hivi ndivyo ionekanavyo Gari hiyo baada ya kupiga mweleka huo.
 Mdau akionyesha kibao cha namba cha Gari hiyo ambacho kiling'oka na kuingia mtaroni.
 Wasamalia wakiengelea kuhakikisha kama kuna mtu mwingine ndani ya Gari hiyo. 
 Majeruhi wakipakiwa kwenye Gari tayari kwa kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
Gari iliyowapakia Majeruhi hao ikiondoka eneo la tukio.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Poleni kwa ajali. Ila watanzania katikati ya mitaa TUACHE kuendesha kwa speed kwanini hatupendi kufuata sheria?? ajali hazitakaa ziishe, mtu anakuwa na harak aya kwenda wapi?? na barabara zenyewe ndio hizo. Tunasema nchi za nje ajali si nyingi kwa kuwa waanafuata sheria.

    ReplyDelete
  3. Jamani Ambulance hakuna siku hizi, Yaani mtu anagongwa halafu mwampeleka na pick up, basi mgetumia saloon car

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...