Ndugu zangu waandishi wa habari, nimewaiteni hapa kwa dharura, ili kuweza kuwafahamisha hali halisi ya mauaji yaliyotokea katika siku za hivi karibuni katika mkoa wa Kipolisi wa Tarime Rorya.
Mnamo tarehe 26 Januari, 2014 majira ya saa 12.00 asubuhi huko katika kijiji cha Mogabiri katika mkoa wa kipolisi Tarime Rorya, jambazi asiyefahamika kwa jina aliwaua kwa risasi Zakaria Mwita Marwa miaka 28 na Erick Lucas Maranya miaka 24 baada ya kukutana nao njiani.
Siku hiyohiyo, majiara ya saa 4:00 usiku, katika kijiji hichohicho cha Mogabiri, jambazi huyo alimuua Robert Kisiri miaka 45 baada ya kuvamia Grocery inayomilikiwa na Chacha Ryoba na kumjeruhi mtu mwingine mmoja.
Tarehe 27 Januari, 2014 majira ya 11:30 alfajiri katika kijiji cha Mugabiri, jambazi huyo alifanya mauaji tena kwa kumpiga risasi David Mwasi Matiko miaka 39 na kumpora simu yake aina ya Nokia. Katika tukio hilo, pia, alimjeruhi Machungu Nyamahemba miaka 19 ambaye bado amelazwa katika hospitali ya Tarime kwa Matibabu.
Siku hiyohiyo ya tarehe 27 Januari, 2014 majira ya saa 2:00 usiku katika kijiji cha Nkende, jambazi huyo alimuua kwa kumpiga risasi Juma Marwa Nyaitara miaka 30. Baada ya kufanya mauaji hayo, jambazi huyo aliwapora simu zao za mkononi Chacha Magige na Masero Marigiri wote wa kijiji cha Nkende.
Usiku wa kuamkia tarehe 28 Januari, 2014, jambazi huyo aliendelea kuua watu wengine watatu ambao bado majina yao hayajafahamika. Mtu mmoja alipigwa risasi wakati akiendesha pikipiki katika kijiji cha Nkende na wengine wawili waliuawa baada ya kukutwa na jambazi huyo wakiwa wanatengeneza gari lililokuwa limewaharibikia katika kijiji cha Mogabiri.
Hadi sasa juhudi kubwa za kumsaka jambazi huyo zinaendelea kufanyika na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi.
 Aidha, mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernesti Mangu, ametuma timu maalum kutoka makao makuu ya jeshi la Polisi inayohusisha kamisheni ya Oparesheni, Upelelezi na Intelijensia kwenda kuongeza nguvu katika juhudi zinazofanyika na ngazi ya mkoa kuhakikisha kwamba, jambazi huyo anakamatwa upesi ili kuondoa hofu kwa wananchi.

Jeshi la Polisi nchini, linatoa wito kwa wananchi wote kutoa ushirikiano ili jambazi huyo aweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria haraka. Mwananchi mwenye taarifa za mhalifu huyo anaweza kutumia namba ya simu ifuatayo 0754 785557.

Mkuu wa Oparesheni wa Jeshi la Polisi,
 Kamishna Paul Chagonja 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ushirikiano zaidi unatakiwa kati ya Jeshi letu la polisi na raia ili taarifa zifikishwe polisi kabla ya kuibuka kwa madhara makubwa kama haya....

    Haiwezekani jambazi linauwa watu kiasi hiki tena si kwa mara moja ni kwa wakati na majira tofauti na bado anaendelea tu bila kuguswa na mkono wa sheria....

    Hii inaonyesha aidha Jeshi letu haliko vizuri ktk kuzikabi dharura au ndo hivyo utoaji taarifa wa matukio ya uharifu umegubikwa na dhana ya uoga na hivyo wananchi kuyanyamazia na haya ndiyo matokeo yake....inaonekana kazi bado iko kubwa!

    ReplyDelete
  2. Yaelekea huyo si jambazi lakini yaelekea kuwa ni kichaa.Inafaa ashughulikiwe kwa gharama yoyote la si hivyo atateketeza zaidi.

    ReplyDelete
  3. The mdudu,hizo ndio faida za kuluhusu watu kumiliki bunduki ovyo ovyo mbona enzi za Nyerere kurikua shwali kabisa,huyo sio jambazi mbona anauwa kwa kitu simu huyo atakua kichaa 2 na vip nyie polis mnajua sn kuhesabu watu aliouwa mbona nyie polis mko wengi wakati huyo mnaemwita lijambazi yuko 1 ? Kamateni hilo lijambazi haraka sn bwana kabla halijaleta mazara makubwa

    ReplyDelete
  4. It doesn't make sense..jambazi anaua mara 2 au tatu na zaidi hakuna hata police kujitokeza. Acheni heresha polisi. Afu Tanzania mbona mauaji kila kukicha.....shida nini? Msitudanganye kabisa!!!

    ReplyDelete
  5. hii sio haki kabisa Jambazi anafanya mambo kama haya na kanda maalum ipo what do you think????
    polisi wanasumbua raia tu mbona ukiwa unapita hapo polisi wanakusimamisha na kukagua gari lako je inamaana walikuwa wapi
    jeshi letu lifanye kazi yake maana wapo kimaslahi zaidi hasa hapa tarime

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...