Meneja Habari na Mawasiliano
wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Promosheni yao mpya kupitia Bia ya Castle Lite ya kupata washindi 12 watakaokwenda nchini Afrika Kusini kushuhudia onyesho kubwa la msanii
maarufu duniani,Timothy Zachery Mosley kwa jina Maarufu anafahamika kama TIMBERLAND,Promosheni hiyo itaendeshwa kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia leo Januari 20 mpaka Machi 30.Kulia ni Meneja wa Bia ya Castle Lite,Victoria Kimaro.
Meneja wa Bia ya Castle Lite,Victoria Kimaro akisisitiza jambo juu ya namna wateja wa bia hiyo watakavyoweza kushiri kwenye Promosheni hiyo,ambapo amesema mteja atatakiwa kununua bia hiyo ya chupa na atakapoifungua ataona namba zilizowekwa ndani ya
kizibo na atatakiwa kutuma jina lake na namba hiyo
kupitia ujumbe mfupi wa simu kwenda kwenye
namba 15499.
Meneja wa Bia ya Castle Lite,Victoria Kimaro akionyesha namba itakayokuwa inatumika kwenye Promosheni hiyo.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...