Mmoja wa wanachama watatu wa CHADEMA waliovuliwa nafasi zao za uongozi ndani ya chama, Zitto Kabwe kupitia kwa Wakili wake, Alberto Msando,jana ameanza kufanya ‘FORUM SHOPPING’ kwa kupeleka maombi Mahakama Kuu ya Tanzania, akiomba Kamati Kuu isijadili na kuamua jambo lolote kuhusu uanachama wake, kwenye kikao maalum kinachofanyika leo.
Awali muombaji kwa namna ambayo inaweza kuitwa kuwa ni kuvizia, alitaka Mahakama Kuu hiyo itoe amri kutokana na ombi lake hilo, bila upande wa chama kuwepo mahakamani, lakini kwa bahati nzuri mawakili wa chama, Mwanasheria Mkuu wa chama, Tundu Lissu na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu, Peter Kibatala; wakafanikiwa kuwepo kortini, hivyo wakawa-served maombi hayo kisha mahakama ikalazimika kusikiliza Preliminary Objections (PO) kutoka kwa mawakili wa CHADEMA dhidi ya waleta maombi.
Maombi hayo ya wakili Msando kwa niaba ya Zitto yamefunguliwa mahakamani dhidi ya Baraza la Wadhamini CHADEMA na Katibu Mkuu wa Chama.
Hoja za mawakili wa CHADEMA katika PO zilikuwa ni katika maeneo matatu ambayo ni vifungu vya kisheria ambavyo waombaji walikosea;
1. Vifungu vya sheria walivyotumia waombaji kuomba court injunction, haviipatii Mahakama Kuu mamlaka ya kufanya maamuzi hayo wanayoomba ifanye. Kwa sababu kwa ujumla ukikosea vifungu hasa vinavyohusu msingi wa kesi, ni sawa na kwamba hakuna kesi.
2. Hati ya kiapo ya waleta maombi haikuwa na facts kama inavyotakiwa badala yake ilikuwa imejaa maneno ya ubishi ubishi.
3. Mahakama haiwezi ku-entertain kusikiliza migogoro ya ndani katika vyama vya hiari mf; vyama vya siasa, dini na michezo (ambavyo uanachama wake ni wa hiari), kwa sababu mojawapo ya principle ni kwamba ili mtu awe mwanachama anakuwa amekubaliana na katiba, kanuni, taratibu na makatazo ya chama husika.
Aidha katika maombi yake kuna vitu vingine ‘muhimu’ ambavyo mleta maombi amejikuta akivionesha kuwa anakubaliana na taratibu za chama lakini wakati huo huo tena anataka mahakama imsikilize;
· Amekiri kuwa amevuliwa nafasi za uongozi na amekata rufaa
· Amekiri kuwa ameandikiwa mashtaka kwa maandishi na yeye amejibu
· Amekiri kuwa ameandikiwa kuitwa mbele ya kikao cha Kamati Kuu ili asikilizwe utetezi wake kwa mdomo.
Kwa maneno yake hayo ni kwamba anakubaliana na na process ya chama na kwamba anajua atasikilizwa lakini tena wakati huo huo anataka mahakama imsikilize. Huo ndiyo msingi wa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA kusema kuwa kuhangaika huko ni sawa na kufanya ‘FORUM SHOPPING’.
Mleta maombi angeweza kuwa na hoja katika maombi yake iwapo angeona kuna breach of natural justice kwenye suala lake. Kitu ambacho hakijatokea na hata yeye kwenye maelezo yake anakiri hivyo.
Uamuzi wa Mahakama Kuu
Katika uamuzi wake, Jaji Utamwa amesema chama kitaendelea na shughuli zake kama kawaida.
Hivyo kikao maalum cha Kamati Kuu kilichopangwa kufanyika kesho Januari 3, 2014, kitafanyika na kitajadili agenda zote (kama zilivyotolewa awali) na masuala yote yanayohusu uendeshaji wa chama, isipokuwa hakitajadili na kuamua kuhusu uanachama wa Zitto pekee, hadi Mahakama Kuu itakaposikiliza ombi lake kesho saa 3 asubuhi.

Imetolewa na-
Kurugenzi ya Habari-Chadema

The mdudu,sisi kama wananchi wa kawaida wala hatujui tuanzie wapi coz hatujui kiundani huo mgogoro ulianzia wapi na ni nn chanzo chake ila nyie wakuu wetu ndio mnaojua ulipoanza na ulipo na unakokwenda so busara itumike ili uishe huo mzozo kisha tujiandae na uandikaji wa KATIBA YETU YA TANGANYIKA why nasema hivi? Coz mnatuchanganya sisi wananchi wa kawaida tusio igemea kwenye siasa au malumbano yasio na faida kwenye jamii yetu.
ReplyDeleteToo low, yaani hii ndio inaitwa kurugenzi ya habari? hii inaonyesha ni kwa kiasi gani watu wanaotaka tuwaamini, hawaaminiki, huwezi ukasimamia demokrasia wakati huo huo hutaki utawala wa sheria. Tangazo hili kwa kiasi kikubwa limeingilia utendaji wa mahakama na kwa kiasi kikubwa limekosa umakini.
ReplyDeleteUlitaka uambiwe nini? hiyo ndiyo habari uliyopewa, too low ni kipi? Usikurupuke tu
DeleteCHADEMA huu ni mwanzo wa mwisho wa chama chenu,inaonyesha jinsi gani mlivyo wanafiki na wazindiki. This is pure no sense, you can not write this bias response thinking we will buy into it. Kila Mtanzania ana haki ya kujitetea mahakamani kwa jambo lolote lile, mahakama itamsikiliza mtu huyo kama haki yake na kutoa maamuzi ya kisheria. To call this is a "Forum Shopping" is cheap politics. This is the matter of everyone's rights and any Tanzania bears that right. Stop being hypocrites.
ReplyDeleteMdau,
N.E
Mtu wa pili kutoka juu...upo makini sana nakupa hongera....nimeisoma hii habari na kuielewa sawa ambavyo wewe pia umeielewa....yaani hapa sasa ni dhahiri...kwamba watu wanapotosha habari ili kupata sapoti tu ila huu si uhalisia......kubwa na la muhimu ni hukumu ya iliyotolewa na mahakama juu ya ombi la...muhusika....haya mengine ni mbwembwe tu kutaka kuwachanganya watu na vifungu vyao vya sheria lakini hakuna kitu......ni sawa na mwanafunzi aliyeandika essay ndeefu lakini point chache au hakuna.......
ReplyDelete