Wakazi wa maeneo mbali mbali ya jiji la Dar wakiwa kwenye kituo cha basi cha Mbezi mwisho asubuhi hii kusubiria usafiri wa kwenda mjini Dar es salaam kwa shughuli mbalimbali. Hali kama hii utaikuta maeneo ya Mbagala, Temeke Mwisho na kweingineko katika muda huu. Jioni halihii huonekana Posta Mpya, Mnazi Mmoja na Msimbazi. Je, nini kifanyike kupunguza adha hii? Na hao ni abiria wa mabasi, bado wenye magari binafsi na usafiri mwingine, wote wakielekea katikati ya jiji.
Kibaha Picha ya Ndege
Nyomi ya Mbezi Mwisho
Hapa ni Mbezi Mwisho asubuhi hii





.jpg)
Hakika hatukuwa makini sana kuwa na dira ya kupanua barabara na kuwa na mradi wa mabasi yaendayo kasi hadi Kimara mwisho, labda ilistahili angalau hapo Mbezi mwisho! Tujitahidi kuwa na VISION pana kwa ajili ya maendeleo ya kweli!
ReplyDeletekazi kweli kweli
ReplyDeleteserikali iache kujenga na kuendelesza kila kitu city centre wapeleke mikoa mingine sio lazima kila kampuni iwena hqrt dar na ni vile vile sio kila biashara/kampuni ziwe city centre ya Dar waanze kuiga nchi nyingine tambazeni maendeleo sio dar tu
ReplyDeleteTATIZO SIO VISION, TATIZO NI UFISADI, HAPO HAPO MTU ANATAKA ABANIE ACHUKUE HELA ZINGINE AWEKE MFUKONI
ReplyDeleteBongo tambarareeee.
ReplyDeleteTreni za mjini Bongo ziongezwe ndiyo suluhu ya kero hii.
Mdau
Jijini N.Y
Eee viongozi Tanzania amkeni huduma zisambazwe kila pahali sio zote ziwekwe mahali pamoja, kama maofisi zijengwe kila eneo staili kupunguza kero kama hii kwa wananchi na pia ni wepesi wa maendeleo. Angalia hapo unategemea mtu atafika ofisini saa ngapi? Akifika ofisini itakua saa7 mchana ni lunch time atapumzika saa8 saa9 anaondoka tena kuwahi usafiri amefanya kazi masaa mangapi hakuna unakuta kia siku ni hivyohivyo kazi inazorota maendeleo sifuri tunalia nchi masikini
ReplyDeleteNaungana na Wadau wa 3 na wa 6 kuhusu kuzipanua na kuzisambaza Huduma Muhimi nje ya Jiji.
ReplyDeleteNADHANI HUU MUDA TULIO NAO NI MUDA WA KILA KITU DOT.COM hivyo NI KIASI CHA KUZIWEKA HUDUMA MUHIMU KTK VITUO NJE YA JIJI KWA NJIA YA MTANDAO NA TEKINOLOJIA YA KOMPUTA.
INAWEZEKANA KTK RUNDO HILO WAPO WATU WANAO JIKUTA WANATUMIA MUDA, NAULI NA MATUMIZI MENGINE KWA SHIDA KAMA MOJA YA HIZI HAPA CHINI.
1.KWENDA MAKAO MAKUU YA WIZARA KUTAZAMA MAJIBU YA MCHAKATO FULANI IWE KAZI AMA HUDUMA ZA KISERIKALI ALIZOOMBA HAPO KABLA.
2.KUFUATA FOMU (TENA MOJA TU) YA MAOMBI YA KITU KAMA PASIPOTI, LESENI YA BIASHARA AMA FOMU YA KULIPIA KODI.
3.KURUDISHA OMBI LA HUDUMA ZA KISERIKALI KWENYE IDARA YA SERIKALI.
4.KWENDA KUSAINI KTK FOMU YA BENKI KUIDHINISHA FEDHA KUTOLEWA KTK AKAUNTI YA BENKI.
5.KWENDA KUPELEKA PICHA TU BAADA YA KUOMBA HUDUMA FULANI NA KUPELEKA BARUA YA OFISI YA TENDAJI WA KATA.
(MAMBO HAYO YOTE MATANO 5 NA MENGINE ZAIDI YA HAYO YANAWEZA KUFANYWA KIDIJITALI TENA KWA UFASAHA NA UFANISI ZAIDI, PIA BILA KUSHIRIKISHA SUALA LA RUSHWA AMA UPENDELEO)
Kwa njia hiyo ndio hiyo adha inayooneka hapo itakwisha!
Ala nyie watu wa Kimara na Mbezi mnatucheka watu wa Mbagala kupandia madirishani ktk mabasi!
ReplyDeleteJe, hapo kwamjazano huo likitokea basi mtasema hamtapandia basi madirishani?
Duuu kama ni hivyo hata kwa nyumba y bure sikai Mbezi na Kimara !
ReplyDeleteNi vile hakuna njia ya short cut kuingia Jijini kutokea Kimara na Mbezi ni lazima unyooshe na Barabara ya Morogoro moja kwa moja.
Si bora kukaa Keko Toroli ama Keko Magurumbasi ukizama bondeni unaibukia Karikaoo na Gerezani?