BONDIA asiye na mpinzani Tanzania Francis Cheka, anatarajia kupanda ulingoni tena Februari 8 kuwania mkanda wa uzito wa kg 82(Light Heavy weigh) akichuana na Mrusi Valery Brudov.

Cheka miungoni mwa mabondia wenye rekodi nzuri licha ya hivi karibuni kuharibu rekodi yake kwa kupigwa na Fedor Chidinov wa Russia na kupokonywa mkanda wa ubingwa wa Dunia WBF alioupata Agost mwaka jana kwa kumchapa Phil Williams wa Marekani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Promota wa pambano hilo Jay Msangi ambaye pia alikuwa promota wa pambano la awali alisema, ameamua kumwandalia Cheka pambano hilo kali pia ili aweze kuendelea kujenga rekodi yake kikamilifu.

Msangi alisema, pambano hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam siku hiyo, kwani anaimani pambano hilo litaendelea kujenga heshima ya bondia huyo hapa nchini licha ya kupoteza mkanda wake hivi karibuni.

 ALisema, licha ya kukutana na changamoto mbalimbali katika pambano lilopita, ila yeye dhamira yake ni kuendeleza mchezio huo hapa nchini na ndio sababu ya kuleta mabondia wenye uwezo mkubwa kupambana na Cheka.

“Bondia huyu ana uwezo mkubwa sana nchini kwao, kwani amecheza mapambano 42 kashinda 39 huku akishinda KO 28 na kupoteza mitatu tu,”alisema Msangi na kuongeza kuwa, Bondia huyo ni bingwa wa Dunia wa zamani wa WBA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...