Na Abdulaziz Lindi

Shule Nne za kata kati ya shule 115 za sekondari zilizopo mkoani Lindi zimekosa wanafunzi wa kidato cha kwanza 2014 kutokana na kukosa wanafunzi wa kujiunga na shule hizo.

Hayo yameelezwa na Afisa elimu wa mkoa wa Lindi Silas Samaluku wakati alipokuwa anatoa taarifa ya maendeleo kwa wajumbe wa kikao cha wadau wa elimu Mkoani Lindi.

Samaluku alisema kuwa Mkoa wa lindi una jumla ya shule za sekondari 115 na wanategemea wanafunzi wote waliofaulu watajiunga katika na shule hizo lakini shule nne za sekondari kati ya hizo Namapwia na Kilimarondo za wilayani Nachingwea ,Madangwa wilayani Lindi na Nandanga wilayani Kilwa zitakuwa hazina wanafunzi wa kuanza kidato cha kwanza 2014 kutokana na kukosa wanafunzi wa kujiunga na shule hizo

Alieleza kuwa wanafunzi 17,249 walisajiliwa kuhitimu elimu ya msingi kati ya hao wavulana ni 7,981 na wasichana 9,448 lakini kati yao waliofanya mtihani ni 16,682 na wasichana 9,150 sawa na asilimia 95.71.

Wanafunzi waliofaulu na kupata alama 100 hadi 250 walikuwa 6,857 kati ya hao wavulana 3,644 na wasichana 3,213 sawa na asilimia 41.1 ambayo imepanda ukilinganishwa na mwaka 2012 ambapo ilikuwa asilimia 22.60 .

Aidha Samaluku alibainisha kuwa kipindi cha miaka miwili mfululizo wanafunzi wa wilaya ya liwale wanaongoza kwa kufanya vizuri mitihani ya darasa la saba kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa.

" mwaka 2013 Liwale imeongoza kwa kufaulisha kwa asilimia 53.37 ikifuatiwa na wilaya ya Nachingea kwa asilimia 50.05 ,Lindi manispaa kwa asilimia 42.42 wilaya ya Ruangwa kwa asilimia 42.34 ,Kilwa asilimia 33.74 ,wakati huo Lindi vijijini ikiendelea kushika mkia kwa muda wa miaka miwili mfululizokwa kuwa ya mwisho kupata asilimia 31.45

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...