Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Titus Kamani, amesema ili kwenda na
kasi ya maboresho ya wizara hiyo, inahitajika dhana ya uwajibikaji na uwazi sambamba
na kujitolea kwa nguvu zote katika kufanya kazi.
Waziri Kamani, ameyasema hayo leo katika mkutano wa kwanza uliowakutanisha
wafanyakazi wote wa wizara hiyo, wakiwemo wastaafu wa mwaka jana katika ofisi za
wizara hiyo zilizopo Temeke jijini Dar es Salaam.
Amesema kama kuna mtu ambaye ni kikwazo katika kukwamisha shughuli za wizara, ni
bora akawapisha mapema na kwamba kila mtumishi kwa nafasi yake, anatakiwa kuifanya
kazi kwa uwazi na akaitaka wizara kufanya kazi na vyombo vya habari kwani ndio njia
pekee ya kuwafanya watanzania wajue wizara inafanya nini.
“Wewe upo ofisini, halafu unaogopa ogopa vyombo vya habari, kwani unatatizo gani,
kuweni wazi mambo yenu yawe hadharani, watanzania wa Mbeya wayajue, Rufiji mpaka
Pemba, hakuna kufichaficha jambo katika wizara yangu.” Alisistiza Dk Kamani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...