Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Bw. Morice Oyuke kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu ukuaji wa Pato la Taifa kwa robo mwaka ya tatu ya mwaka 2013 ambapo katika kipindi cha Julai – Septemba, 2013 Pato la Taifa kwa bei za soko liliongezeka kwa kasi ya asilimia 6.5 ikilinganishwa na asilimia 7.2 kwa kipindi kama hicho mwaka 2012. Kulia kwake ni Bw. Juma Omary, Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Tume ya Mipango na kushoto ni Bw. Daniel Masolwa Meneja Takwimu za Pato la Taifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Bw. Morice Oyuke kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (katikati) akizungumza kuhusu ukuaji wa Pato la Taifa kwa robo mwaka ya tatu ya mwaka 2013 katika ukumbi uliopo Ofisi ya Rais Tume ya Mipango, Dar es Salaam. (Picha na Veronica Kazimoto).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...