Na Hassan Mndeme na Tumaini Julius – Jeshi la Polisi
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe, Emmanuel Nchimbi ameahidi kushirikiana na Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi katika kuihimiza Serikali kuongeza bajeti ya wizara hiyo kwani anafahamu umuhimu wa wizara hiyo na changamoto zinazoikabili.
Alisema hayo kwenye kikao kilichofanyika jana Makao Makuu ya Jeshi la Polisi baada ya makabidhiano na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa waziri wa wizara hiyo.
Aliongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ni wizara muhimu katika mustakabali wa amani ya nchi hivyo ikiwa na bajeti ya kutosha itaweza kuwajengea watendaji mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na kuboresha maslahi yao na kuongeza ufanisi, uaminifu na uadilifu katika utendaji wao wa kila siku.
Aidha, alisisitiza kuwa misingi na wajibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni kutoa haki kwa raia, wizara ikikalia haki nchi haitakalika, hivyo raia wanapaswa kupewa haki zao kwa wakati unaostahili kwani ni njia mojawapo ya kujenga ushirikiano na jamii na kuzuia uhalifu kabla haujatokea.
Pia, Mhe Nchimbi amewataka wananchi kufuata sheria katika kutafuta haki zao badala ya kujichukulia sheria mkononi na kuwa serikali itawachukulia hatua za kisheria watu wote watakaobainika kushiriki katika vitendo vya kihalifu.
Awali akimkaribisha aliyekuwa waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe, Mathias Chikawe alihaidi kutoa ushirikiano kwa kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kutoa haki kwa raia kwa wakati unaostahili bila upendeleo ili kutoa uduma bora kwa wananchi.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Amme Silima amewataka watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kufanya shughuli zao kwa kufuata maadili, sheria na kanuni za kazi zao ili wananchi waweze kupata huduma wanazostahili.
Silima aliongeza kuwa miongoni mwa changamoto zinazoikabili Wizara ya mambo ya ndani ni ufinyu wa bajeti, tabia za wananchi kujichulia sheria mkononi, matukio ya kufunga Barabara, mauaji ya kulipiza visasi au kuadhibu watu wanaotuhumiwa kuwa wahalifu na kusema vitendo kama hivyo havipaswi kuvumiliwa kwa vile vinaweza kusababisha machafuko makubwa hivyo wizara inapaswa kuandaa mikakati ya haraka ya kukabiliana na hali hiyo kabla haijasababisha madhara makubwa katika jamii.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Pereira Amme Silima, Naibu Katibu Mkuu Ndugu Mwamini Juma Malemi, makamanda wa Vyombo vya dola vilivyopo Wizara ya Mambo ya Ndani na wakuu wa idara hiyo.
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe, Dkt Emmanuel Nchimbi akizungumza jana na wakuu wa idara za wizara hiyo baada ya kukabidhi rasmi ofisi kwa Waziri Mathias Chikawe aliyeteuliwa na Rais hivi karibuni kuongoza Wizara ya Mambo ya Ndani. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
aliye juu mpandiye huko huko!
ReplyDeletemdau vancouver
Ahsante Mhe.Dr.Nchimbi!
ReplyDeleteIsipokuwa ningefurahi sana kama utashiriki ktk OPERESHENI KIMBUNGA ukiwa kama Mbunge licha ya kuwa sio Waziri kwa sasa.
Ni kuwa Afrika ya Mashariki imepata salamu na kumtambua sana Mhe.Nchimbi kwa jinsi alivyoendesha Operesheni zake!
Nina hakika wanakufahamu vizuri sana nchi za Rwanda ,Uganda, Burundi, Congo-DRC, India, Somalia ,Ethiopia , HATA NCHI ZA WAZUNGU KWA RAIA WAO WALIOKUMBWA NA KIMBUNGA KAMA ITALY, NORWAY, UJERUMANI NA USWISI WATAKUKUMBUKA SANA!
ULITISHA SANA HADI KUWAKAMATA WAZUNGU UHAMIAJI HARAMU KTK OPERESHENI?
Ohhh!
ReplyDeleteMzee wa Operesheni Kimbunga Dr.Nchimbi ndio unatundika daruga?
Lakini ingekuwa vyema ukamwachia Dozi Mhe. Chikawe aiendeleze!