Kocha Mpya wa timu ya Yanga, Hans Plujim akiwa kwenye uwanja wa Ndege wa J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam kabla ya kukwea pia kuwafuata wana Jangwani huko nchini Uturuki wanakoendelea na mazoezi yao ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara. Kocha huyo aliondoka jana alasiri kwenda nchini Uturuki kujiunga na Kocha Msaidizi wa timu hiyo,Charles Boniface Mkwasa na kikosi kizima cha Yanga.Kocha huyo ambaye amesaini mkataba wa miezi sita ya awali na klabu hiyo,amesema amejipanga vyema kukinoa kikosi hicho pamoja na mambo mengi mno kwa klabu hiyo,ambapo pia amesema anamjua vizuri kocha wa Simba Logarusic ambaye mwaka 2012 alimchapa kwa mabao 4-1 wakati huo Plujim akifundisha Berekum Chelsea ya Ghana na Loga akiwa Ashanti Goldb SC. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kwa hiyo Kocha mpya Yanga anatuhakikishia Wanajangwani kwa Mabao aliyowahi kumchapa Kocha wa Simba huko Ghana ina maana Mnyama tutamzamisha kisu cha shingo sio?

    Lakini asije akatafuta pa kutokea kama ahadi hiyo ikiyeyuka na tukafungwa na Simba!

    ReplyDelete
  2. Kwani kocha lazima awe Mzungu Jamani,Mbona sisi watanzania hatuaminiani. Boni yupo mmpeni nafasi basi, duuh bado ukoloni mamboleo unatupeleka, Sijui tutajifunza lini?

    ReplyDelete
  3. Kocha si lazima awe mzungu Ila its a sign of luck of self confidence and esteem on the part of the Management team of Yanga and many local clubs - Emulate Nigeria- the champions of Africa and AC Milan (Seedof)

    ReplyDelete
  4. Na bado ataletwa balozi wa nyumba kumi mdhungu teh teh teh

    ReplyDelete
  5. Kwahiyo yanga itaipika 4-1 simba? Huyu sio kocha nawaambieni. Anafafanisha uwezo wa kocha kwa vigezo kama hivyo!
    Mtamsikia,huyu ni maneno mengi kama yanga wenyewe, uwanjani hawana lolote.

    ReplyDelete
  6. kachooooooka!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...