Mkuu wa mkoa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi amewataka vijana kutambua kuwa kwa sasa sanaa ni ajira na ni fursa nzuri ya kujiongezea kipato tofauti na ilivyozoeleka kwenye jamii kuwa sanaa inalenga kutoa burudani na hivyo amewataka vijana hao kuichangamkia fursa hiyo.

Rai hiyo ilitolewa mapema jana wakati mkuu huyo wa mkoa alipotembelea kambi ya jeshi 834 KJ JKT MAKUTUPORA Dodoma kukagua shughuli za kikundi kipya cha sanaa ya ngoma za asili kilichoanzishwa na kikosi hiko cha jeshi. Dr Nchimbi aliwataka vijana kwa kutambua umuhimu huo wa sanaa hawana budi kuongeza bidii, kufanya mazoezi zaidi ya kuimba,kucheza. 

Aidha amewataka vijana kufanya utafiti zaidi wa tamaduni za jamii mbalimbali za kitanzania, nyimbo zao za asili, uchezaji wao na hata Mavazi yao na kuwa ili waonekane na kufahamika zaidi wajitahidi kushiriki kwenye matamasha mbalimbali ya sanaa na matukio yanayojumuisha burudani za sanaa.

Aliongeza kuwa kwa sasa sanaa hasa nyimbo za asili zinakuza utamaduni, lugha zinamtangaza mtu na taifa lake hadi kwenye nyanja za kimataifa. Amewataka vijana hao wanaounda kundi hilo la ngoma za asili kuboresha kazi yao na kuhakikisha inaendelea kufanya kazi ya kutoa elimu, kuhimiza kazi za uzalishaji,kukemea uovu na uvunjifu wa taratibu na kanuni katika jamii na wakati swingine hata kuhifadhi historian.

Kwa upande wake kamanda wa kikosi cha jeshi 834 KJ JKT Makutupora Luteni Kanali Fuime akiwasilisha taarifa kwa Mkuu huyo wa mkoa amesema mojawapo ya kazi ya JKT ni kufundisha uzalendo na utamaduni wa kitanzania na kusema kuwa kikundi hiko kipya cha sanaa za ngoma za asili kinafanya kazi kubwa  ya kufundisha vijana tamaduni za jamii za kitanzania.Na

Amesema kuwa katika dunia ya sasa vijana wengi wanazaliwa na kukulia mijini mahala ambapo hawapati fursa ya kujifunza tamaduni za jamii za kitanzania  hivyo vijana watakao pitia mafunzo ya JKT hapo makutupora watakua wanapata fursa ya kujifunza mambo hayo muhimu kupitia kikundi hiko kipya cha sanaa za ngoma za asili.
Mkuu wa mkoa dodoma Dr. Rehema Nchimbi akipokea salamu ya kijeshi mara baada ya kuwasili Kambi ya jeshi 834 KJ JKT Makutupora mapema jana kukagua kikundi kipya cha sanaa za ngoma cha JKT Makutupora.
Mkuu wa mkoa dodoma Dr. Rehema Nchimbi akipanda mti wa mzabibu kwenye eneo la kambi ya jeshi Makutupora kama ishara ya kumbukumbu alipotembelea kambini hapo jana kujionea shughuli za sanaa ya ngoma kutoka kwa kikundi kipya cha sanaa za ngoma cha JKT Makutupora.
Mkuu wa mkoa dodoma Dr Rehema Nchimbi (kushoto) akiongozana na kamanda wa kikosi 834 KJ Makutupora Luteni Kanali Fume (katikati) na Kaimu Mkuu wa shule ya kijeshi Makutupora Meja Ruwa (kulia) wakielekea bwalo la jeshi kambini hapo kukagua shughuli za sanaa za kikundi kipya cha sanaa ya ngoma cha JKT MAKUTUPORA MAPEMA jana.
Kikundi kipya cha sanaa ya ngoma za asili cha JKT MAKUTUPORA Dodoma kikitumbuiza nyimbo ya asili ya wenyeji wa mtwara mbele ya mkuu wa mkoa dodoma (hayupo pichani) mapema jana wakati mkuu huyo wa mkoa alipofika kambini hapo kukagua shughuli za kikundi hiko kipya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...