Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Oman (Tanzania Club in Oman-TANCO) ilifanya mkutano wake mkuu hapo Ijumaa tarehe 17.01.2014 mkutano uliohudhuriwa na watanzania jumla ya 150 wanaoishi na kufanya kazi nchini Oman.
Katika Mkutano huo Mwenyekiti wa TANCO ndugu Hassan Wazeer Mtonga alitumia mkusanyiko huo kutafuta usahihi wa habari zilizoenea pamoja na picha zikionyesha wanawake wawili wakiwa wameungua na kudai kuwa ni wadada Kakitanzania na kuwa wamefanyiwa ukatili huu na mabosi wao wa Oman.
Ndugu mtonga alieleza kuwa alizipata taarifa hizo na yeye kwa nafasi yake ya Uenyekiti aliziwasilisha Ubalozi wa Tanzania nchini Oman ambao nao walizifanyia kazi kushirikiana na Serikali ya Oman kupitia polisi, hospital na viwanja vya ndege, lakini taarifa hazikuonesha kuwepo kwa tukio hilo na kuthibitisha kuwa ni uzushi na uongo kwani hawakuweza kupata majina ya watanzania hao, waajiri wao na mazingira ya mashambulio hayo.
Ndugu Mtonga aliwaomba Watanzania wote waliohudhuria Mkutano huo ambaye anataarifa sahihi kuhusu matukio hayo aziwasilishe , lakini hakuna hata mmoja aliekiri kuwa na taarifa kamili zaidi ya kupokea picha hizo kupitia mtandao wa Whatsapp.
Mwenyekiti alisisitiza kuwa habari ile si ya kweli na kwamba ni uzushi usio na misingi yeyote ambao unaweza kuwa na athari kubwa katika mahusiano ya nchi.
Mwenyekiti alieleza kuwa habari hii ya uvumi wa kuunguzwa na kumwagiwa tindikali kwa watanzania haikupokelewa vizuri na wenyeji wetu wa Oman na kuwa inatishia kuharibu uhusiano wa kindugu na kihistoria uliopo baina ya Tanzania na Oman na pia watanzania na waoman kwa kupelekea kuzuiwa kwa watanzania kuja Oman kufanya kazi na hivyo kushindwa kutumia fursa za ajira zinazopatikana Oman.
Mwenyekiti aliwaasa watanzania kuwa makini na matumizi ya mitandao na kuepusha kutumia mitandao kusambaza habari ambazo si za kweli. Aliwaomba kuwa habari yeyote inayomuhusu mtanzania mahala pa kuanzia ni ubalozini au kwenye Jumuiya ya Watanzania nchini Oman.
Mwenyekiti pia aliwasihi wa Tanzania kufanya kazi kwa juhudi, maarifa na nidhamu ili kuijengea sifa nzuri Tanzania.
Aliwakumbusha Usia wa Rais Jakaya Kikwete alipokutana na watanzania wanaoishi Oman wakati alipotembelea Oman mwaka 2012 alipowausia watanzania kuwa raia wema na kujiepusha na vitendo vya uvunjaji sheria za nchi wanamoishi.
Aliwakumbusha Usia wa Rais Jakaya Kikwete alipokutana na watanzania wanaoishi Oman wakati alipotembelea Oman mwaka 2012 alipowausia watanzania kuwa raia wema na kujiepusha na vitendo vya uvunjaji sheria za nchi wanamoishi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya watanzania Oman Ndugu Hassan Mtonga( Aliesimama) akiongea na Watanzania katika mkutano mkuu wa Jumuiya watanzania nchini Oman uliofanyika Muscat, Oman Ijumaa tarehe 17 Januari 2014.
Sehemu ya Watanzania wanaoishi nchini Oman wakiwa kwenye mkutano huo.



Whoever disagrees with allegations of modern slavery in that part of the world is either blind, deaf or both! The only explanation may be that one gets so much accustomed to abuse that one fails to recognise it. I can understand that people may want to protect their backs - but in their shoes, I would rather stay quiet than deny that such abuse is rampant. The bottom line is, people are abused and the whole world knows. It is a shame that those closest to the gates of torture can not see it!
ReplyDeleteWhat prove do u have that people are abused in oman?
DeleteAhssante kwa bidii ya kutafuta ukweli; mambo ya kizushi mitandaani ni mengi. Taarifa kutoka kwa mamlaka husika ndiyo ya kuiamini; kama jumuiya ya watanzania waishio Oman mulivyotoa taarifa hii--maana yake ndiyo taarifa iliyokuwa sahihi. Hakuna Mtanzania aliyemwagiwa tindikali; ulikuwa ni uzushi. Yabidi kutafuta chanzo cha hiyo habari, nafikiri kitengo cha mawasiliano kilicho chini ya polisi hapa kwetu Tanzania wanaweza lishughulikia hilo na umpata mhalifu. Tunataka taarifa sahihi ili hatua stahiki zichukuliwe. Tuache kuzusha mambo, dunia tuifanye sehemu nzuri ya kuishi kila mmoja kabla hajahamia upande mwgine mwa maisha yani akhera. kazi njema kaka michuzi
ReplyDeletewewe mdau wa kwanza, hapana aliyekataa, aliye na uthibitisho kama hizo specific cases zimetokea na apeleke ili zishughulikiwe.
ReplyDeleteUsizunguke mbuyu bure.
Kwa kweli ni jambo la kusikitisha sana binadamu anapozua jambo la uongo katika magazeti au mitandao jambo ambalo linasababisha kizaa zaa kwa kila mtu hasa unapokuwa ukiwa katika nchi ambayo inasemwa kuwa tukio hilo limetokea! Mimi nikiwa mtanzania niishie hapa Oman miaka zaidi ya 20 sijapata kutukanwa, kudhalilishwa au kudharauliwa na Mu-Omani kwanza watu wake wakarimu sana! Hapa hata ukiwa huna senti hufi njaa watu watakupa chakula hilo nashuhudia kwa kauli na vitendo bila kusahau Wa-Omani ni ndugu zetu kwa damu historia hawezi mpumbavu mmoja akaibadilisha thats our destiny!
ReplyDeleteHapa kuna sheria na hakuna nunda juu ya sheria ikiwa unadai haki yako utaipata kisheria! Unapoishi katika nchi ya kigeni fuata sheria utaishi bila matatizo. Hapa hakuna magazeti yanaandika habari za "Udaku" yanayoandikwa ni "hard facts" hizo za udaku zina faida gani katika jamii zaidi ya kuongeza ufuska? Nawaomba Waandishi waandike ukweli na porojo waweke kando! Kalamu ni amana kwenye shingo yako kila unachokiandika wewe ndio responsible ikithibitika unaandika uwongo basi ujuwe kamba ya mwongo fupi!
100% I agree" kwa huyo mwenye comment ya kwanza. Bravo!
ReplyDeletemdau holland.
Walioko oman lazima watetee ujinga hata kama unawaathiri kwani tayari waliisha ukubali,wanjua wa -oman wenyewe wakijua kuwa wanalalamikiwa watawafukuza hivyo ni wajibu wao kutetea uhalifu wa waoman wachache.
ReplyDeleteUnyanyasaji upo lakini kwa kuwa wanaogopa kufukuzwa kwa kulaumu wanatetea ujinga huo.Kuna mifano hata marekani enzi utumwa ulipokuwapo kuna baadhi ya watu weusi(watumwa) waliowahi kuwatetea wazungu watwana wakihofiwa kufanyiwa vitu vibaya na mabwana wakubwa hao ikiwa wangegundulika walikuwa wakilalamika kuhusu kunyanyaswa kwao,hili ndilo linalojiidhilirisha hapa, kilio kimewekwa hadharani kunawoga wanaoogopa wantetea upuuzi huu.
Kuna mifano mingi,hata hapa Tanzania kuna ma-house girl wananyanyaswa lakini ikitokea mtu akasema ananyanyaswa ,kwa hofu huyohuyo house girl atakataa kwa nguvu zote kwamba hanyanyaswi na hajawahi kulalamika kokote, atakwenda mbali kuwashutumu hao wanosema ananyanyaswa kuwa waongo yeye hajawahi kulalamika popote.Maanayake ni kwamba house girl huyo anaogopa mwenye nyumba akisikia kashfa hizo anaweza kumfukuza kazi,ili khali huyo house girl hana pakwenda na hana altenative.kwa mfano huo utaona ni jinsi gani hao ma house girl na ma house boy wa oman wanatumia nguvu kupinga kunyanyaswa,ili wasiwachefue wa oman,ukweli ni kwamba manyanyaso yapo,uoga ndo unao onekana katika utetezi wao.kuna mmmoja kasema eti kama huna chakula wanakupa,mhmmm kirahisi hivyo hahahaha.
Una ushahidi gani kama hayo manyanyaso yapo?au umeshawahi kuyashuhudia?
DeleteUkisikia khiana na unafiki ndio huo..
ReplyDeleteBinadam wengi kawaida kupenda kuharibu ya wenzao.. Mmeona wanafaidi sana hao kufanikiwa kufanyakazi Oman! Ndo maana mkazusha yaso kichwa wala mguu
Wanadada chungumzima wafanya kazi kwa heshma na adabu na alhamdulilah raha wanayo. Msiwhusudu! Na anaekwenda kwa ujinga akakosa kufanya ujinga ndo atazua hayo.
Mnazua ya uwongo m2vurugie. Ndo majanga yenyewe hayo.. Hakuna cha tindikali wala tindibaridi. Uzushi na uwongo mtupu
Acheni Majanga..
vipi serekali inawapa uhuru waandishi kusambaza khabari zisizokuwa na kithibitisho?
ReplyDeleteHii inaonyesha wazi ni jinsi vipi waandishi wa khabari Tanzania hawana elimu ya kutosha kuhusiana na kazi wanazozifanya,
Tunawaona watu wa Kenya na Uganda kwa sasa wakimiminika kwa kasi sana kuchukua nafasi za kazi nyingi hapa Oman na huenda wakawa ndio substitute.
Kwa sababu wamesoma na kilichowaleta hakuna zaidi ya kutafuta riziki.